Uchakachuaji mafuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchakachuaji mafuta

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nguruvi3, Jul 3, 2010.

 1. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #1
  Jul 3, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
  Hili jambo ni zito na si rahisi kama tunavyoaminishwa. Uchakachuaji wa mafuta ni tatizo la muda mrefu bali sasa limeonekana kuwa kubwa kwa sababu magari ya ikulu yamepata matatizo.

  Kumbukumbu zinaonyesha watu wamelalamikia kuhusu vituo vya mafuta ima kuchezea mashine na kuwadhulumu wateja au kuchakachua. Watu wa daladala wamekuwa wanabeba vidumu ni kwa kukwepa kupimiwa mafuta kidogo. Ukienda kituoni utaambiwa mashine ile mbovu sogeza gari mbele,ukiomba uwekewe katika galoni utarudishwa katika mashine yenye vipimo halisi.

  EWURA wanajua matatizo haya kwa undani lakini hakuna chochote walichofanya,eti juzi wamefungia kituo moshi kana kwamba ndio uhujumu huu umeanza. Wamefanya kazi zao kumpendeza mkubwa ili walinde kazi zao hata kama watanzania maelfu watapoteza maisha.

  Hebu fikiria faini ya milioni 5 ni kitu gani kwa mtu mwenye biashara ya bilioni 1. Kwahiyo hili ni suala la rushwa kuanzia wamiliki ambao wanachangia chama,viongozi wa serikali wanaotoa vibali, Ewura wasioona matatizo hadi magari ya ikulu yazimike, polisi ambao wanakamata madumu ya gongo lakini hililinalogusa maslahi ya mafisadi na viongozi wa serikali kimya. Jiulize mbona hakuna ushabiki kutoka kwa wasemaji wa serikali au bunge,ni kwasababu kila mtu anajua kucheza na matajiri wa tanzania ni sawa na kucheza na serikali.

  Kwa nchi za wenzetu mafuta yakichakachuliwa[kama itatokea] kampuni husika marufuku kufanya biashara hiyo maisha. Kama kwa mfano kampuni ya Mafuta Oil inayoagiza itapewa leseni na jukumu la kulinda mafuta hadi kwa mtumiaji ni nani angechakachua. Hii ina maana msambazi angekuwa anawajibika kwa kampuni na mwenye kituo vile vile kwa kujua kuwa kituo A kikichakachua mafuta kampuni mama inafungiwa. Hakungekuwa na haja ya kuajiri Ewura ambao zaidi ya show up hawana lolote la maana wanalolifanya.

  Lakini tatizo la mafuta linazidi kutuonyesha ni kiasi gani kikundi cha matajiri kinavyo imaliza nchi hii. Hivi serikali itamchukuliaje hatua tajiri yule yule aliyehusika na mkabata fake na hakuwahi hata kushtakiwa. Hivi nani atawajibika kwa serikali kama viongozi wale wale wenye tuhuma wapo CC, NEC na bungeni. Sasa unategemea hukumu gani kama mwizi ni tumbili na hakimu ni nyani.

  Gharama za kutengeneza magari yaliyoharibiwa na mafuta anazibeba mtanzania wa kawaida kwa faida ya viongozi wa serikali wakishirikiana na wahalifu wanaojiita wafanya biashara.

  Hii adhabu ya EWURA ni kiini macho, uchakachuaji ni mradi wa viongozi waandamizi wakishirikiana na wahalifu.Inasikitisha sana. Kwa nchi za wenzetu mkuu wa ewura angekuwa hana kazi siku nyingi lakini kwa vile system ni kulindana, basi mwacheni anajua siri zetu na sisi tumtunze. Kwani haya ni ajabu? Hosea si alitetea Richmond, si bado yupo pale pale, sasa huyu ndiye unategemea amkamate mchakachuaji wa mafuta kwa ''moral authority'' gani. Ticks si tunajua madudu yake lakini PM amefunika hoja bungeni kulinda wenzake,sasa PM ana ''moral authority gani'' ya kumkamata mfanyabiashara anayechakachua mafuta! je kama ni yule wa ticks atasemaje.

  Kiwira si hiyo tunaijua, kwa vile mkubwa yupo basi mazingaombwe yakatokea bungeni hoja ikafa, sasa ni PM au waziri gani atasimamia mafuta ya watu wenye fedha kama hili la kiwira limewashinda.

  Ukiorodhesha uozo wa serikali yetu utagundua kuwa hili la mafuata ni shehmu tu ya miradi ya viongozi na wafanyabiashara wahalifu tena wengi si wazawa, wamenunua passport tu.

  Watanzania tuamke tuwaambie hawa watu ''enough is enough'' tukiwaachia ipo siku wataanza kuuza watoto wetu utumwani. Ukiwa kiongozi tz kama huna roho mbaya huwezi kukaa madarkani hata wiki moja maana ukijua madudu yanayofanyika utapata wazimu.

  Nchi hii ni yetu sote, we must stand up and say no!!
   
Loading...