Uchaguzi Zanzibar gizani

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Aerial-view-of-Stone-Town-620x308.jpg

WAKATI kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani, Zanzibar zikiwa zimeanza, Juma Ali Juma mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amemkatia rufaa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Abdulrazak Khatib Ramadhan mgombea wa Chama cha Wananchi CUF.

Hatua hiyo inatajwa kama mwendelezo wa mbinu za kuhakikisha mgombea wa CCM anapita bila kupigwa na mpinzani wake mkuu katika uchaguzi huo ambaye anatoka CUF.

Juma amekata rufaa hiyo akipinga uamuzi wa msimamizi wa uchaguzi wa Wilaya ya Magharibi ambaye alilitupa pingamizi lake hapo awali dhidi ya Ramadhan.

Katika pingamizi hilo, mgombea wa CCM anadai kwamba mpinzani wake kutoka CUF hakupitishwa na vikao halali vya chama cha CUF hivyo hafai kushiriki katika uchaguzi huo.

Hata hivyo, Fatma Gharib Haji msimamizi wa uchaguzi huo, amenukuliwa akisema, “mgombea wa CCM aliwasilisha pingamizi dhidi ya mgombea wa CUF ambayo yalitupwa, baada ya kuonekana hayakuwa na mashiko. Hatimaye wagombea wote wakapewa fomu za kuwapitisha.”

Fatma amesema utaratibu kuhusu rufaa hiyo unaihusu Ofisi ya Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ambayo ndiyo itakayosikiliza katika muda utakaopangwa.

Awali mgombea wa CUF aliweka pingamizi kuwa mgombea wa CCM akidai kuwa katika kiapo chake hakutaja mali zake. Pingamizi hilo pia lilitupwa na NEC kwa madai kuwa halina mashiko.
 
MBONA KISHWA CHA HABARI NA HABARI ZENYEWE HAZILINGANI
 
Najua kusoma vizuri ndugu, ila wewe hujui kutumia maneno kama yapaswavyo. You need proper education and a training in writting skills
 
Haaaaa....tena nadhani jecha atapewa tena tuzo akifanikisha mbunge kupita bila kupingwa....
 
Najua kusoma vizuri ndugu, ila wewe hujui kutumia maneno kama yapaswavyo. You need proper education and a training in writting skills
Kubali tu, lugha imekupita. Uwakilishaji wa mada unaendana vizuri na maudhui ya kichwa cha habari!
 
Ccm weupe sanaaaa.washukuru wakina Lubavu.La sivyo nchi ingekishaenda upinzani kitambo tu .kikwete mwenyewe alipitishwa kwa JECH'S & LUBAVU'S LAWS.
 
Mfamaji huwa haishi tapa tapa. ....yeye CCM imemshinda hadi aanze kuifuatilia CUF. .??
 
n.e.c isitoe ushindi wa mezani kwa yeyote,tuntaka pambano la mano-a-mano,fist to fist!tunataka tuwachape ukawa mpaka wajute!
 
Umeona uandike na kiingilishi kabisa tujue na wewe wamo
Kabisa mdogo wangu, na utanisamehe kama kuna maudhi. Hao wagombea kila mmoja anajaribu kutumia mbino ya kuweza kupunguza makali ya mwenzie. Na hiyo ni part of playing politics. Tuombe mungu wananchi wapate mbunge mwenye uwezo wakuwaletea maendeleo. Tena tuombe uchaguzi usituletea matatizo na wasimamizi watende haki.
 
Samahani naomba kuuliza, huyo mgombea wa CUF, kapitishwa na upande upi (maalim au lipumba)? I'm Curious.
 
Aerial-view-of-Stone-Town-620x308.jpg

WAKATI kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani, Zanzibar zikiwa zimeanza, Juma Ali Juma mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amemkatia rufaa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Abdulrazak Khatib Ramadhan mgombea wa Chama cha Wananchi CUF.

Hatua hiyo inatajwa kama mwendelezo wa mbinu za kuhakikisha mgombea wa CCM anapita bila kupigwa na mpinzani wake mkuu katika uchaguzi huo ambaye anatoka CUF.

Juma amekata rufaa hiyo akipinga uamuzi wa msimamizi wa uchaguzi wa Wilaya ya Magharibi ambaye alilitupa pingamizi lake hapo awali dhidi ya Ramadhan.

Katika pingamizi hilo, mgombea wa CCM anadai kwamba mpinzani wake kutoka CUF hakupitishwa na vikao halali vya chama cha CUF hivyo hafai kushiriki katika uchaguzi huo.

Hata hivyo, Fatma Gharib Haji msimamizi wa uchaguzi huo, amenukuliwa akisema, “mgombea wa CCM aliwasilisha pingamizi dhidi ya mgombea wa CUF ambayo yalitupwa, baada ya kuonekana hayakuwa na mashiko. Hatimaye wagombea wote wakapewa fomu za kuwapitisha.”

Fatma amesema utaratibu kuhusu rufaa hiyo unaihusu Ofisi ya Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ambayo ndiyo itakayosikiliza katika muda utakaopangwa.

Awali mgombea wa CUF aliweka pingamizi kuwa mgombea wa CCM akidai kuwa katika kiapo chake hakutaja mali zake. Pingamizi hilo pia lilitupwa na NEC kwa madai kuwa halina mashiko.

Natamani hiyo Rufaa dhidi ya mgombea wa CUF isikilizwe na Kailima akisaidiana na Jecha maana hapo najua haki itapatikana bila mawaa!!!!!!!!!!!!
 
Gombea na huyo aliepitishwa , vikao halali vinakuhusu nini? Siasa ikitoweka kichwani kinachobakia ni Si Hasa.
 
Back
Top Bottom