Uchaguzi wa Zanzibar Dec 1963 na Uchaguzi wa JMT Oct 2020 Unatofauti Gani?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,798
71,218
Katika uchambuzi mwingi wa leo kwenye kumbukizi Muungano unakumbusha kuwa kiini cha muungano ni mapinduzi ya Zanzibar 1964 baada ya "Kupokwa" uchaguzi wa Dec 1963 na kumpatia ushindi Sultani badala ya ASP.
Hofu ikawa kuwa huenda Sultani angeweza kurudi hivyo muungano ulikuwa ulinzi kwao.
Sasa tuje kwenye uchaguzi mkuu wa Octoba 2020 ambao ni wazi ulipokwa na kuwapa ushindi 'WOTE' CCM.
Tujiulize, kwa nini mapinduzi baada ya Sultani na chama chake kupora uchaguzi 1963 yanaitwa "mapinduzi matukufu" lakini kupora uchaguzi kwa Magufuli na chama chake CCM 2020 kumenyamaziwa na hakuna "matukufu" yeyote yamefanywa wala hayafikiriwi kufanywa?
 
Mapinduzi ya Zanzibar yalipata baraka ya wenye NCHI Lakini yale ya 2020 hayakupata baraka ya wenye nchi ambao ndio wananchi wenyewe!!
 
Mfano wako unakosa maana uliyoikusidia. Rejea uone kama ina maana unayotarajia.
 
Mleta mada ficha ujinga wako, Acha kufananisha Uchaguzi uliosimamiwa na Malkia na uhuni wa Jiwe
 
Katika uchambuzi mwingi wa leo kwenye kumbukizi Muungano unakumbusha kuwa kiini cha muungano ni mapinduzi ya Zanzibar 1964 baada ya "Kupokwa" uchaguzi wa Dec 1963 na kumpatia ushindi Sultani badala ya ASP.
Hofu ikawa kuwa huenda Sultani angeweza kurudi hivyo muungano ulikuwa ulinzi kwao.
Sasa tuje kwenye uchaguzi mkuu wa Octoba 2020 ambao ni wazi ulipokwa na kuwapa ushindi 'WOTE' CCM.
Tujiulize, kwa nini mapinduzi baada ya Sultani na chama chake kupora uchaguzi 1963 yanaitwa "mapinduzi matukufu" lakini kupora uchaguzi kwa Magufuli na chama chake CCM 2020 kumenyamaziwa na hakuna "matukufu" yeyote yamefanywa wala hayafikiriwi kufanywa?
Mkuu chakaza, mimi nafahamu kwamba Sultan alikuwepo kama alivyo Malkia wa Uingereza na kwenye upande wa siasa kulikuwa na vyama vingi kama vile ZPPP, ASP, Umma Party na ZNP. Katika uchaguzi huo inasemekana ASP ilishinda lakini haikuwa na majority na ZPPP na ZNP (Hizbu) wakaungana na kuunda Serikali chini ya Waziri Mkuu Sheikh Shamte. Hawa ZPPP na ZNP inaamika walikuwa na wafuasi wengi wenye asili ya kirangi rangi na hivyo wakawa wanahusishwa na Sultan. Sultan hakushiriki kwenye uchaguzi kwa kuwa yeye alikuwa Mkuu wa Dola na uchaguzi ulikuwa kwa ajili ya kutafuta Mkuu wa Serikali.
Menhine tuendelee kutafuta historia.
 
Back
Top Bottom