Sele Mkonje
JF-Expert Member
- Oct 2, 2011
- 643
- 846
Kampeni za Uchaguzi wa Mitaa nchini Afrika ya Kusini zimekamilika rasmi siku ya Jana ambapo tumeshuhudia Vyama vyote vya siasa vikifanya kampeni zake za mwisho katika miji mikubwa tofauti hapa nchini. Uchaguzi wa mwaka huu unatarajiwa kuwa na mvutano mkubwa hasa baada ya ANC kutangaza nia yake kubwa katika uchaguzi huu ni kulichukua tena Jimbo La Western Cape hasa jiji la Cape town ambalo lipo chini ya serikali ya DA. Tofauti na miaka iliyopita mwaka huu chama kipya chenye umribwa miaka 3 EFF kimekuja juu kwa kuweka wagombea wake katika kila mtaa nchi nzima kitendo ambacho hakikuwahi kufanywa na chama pinzani cha DA ambacho kina zaidi ya miaka 20 na Hakikuwah kusimamisha wagombea nchi nzima.
Mimi kama mtanzania ninaeishi hapa Afrika ya kusini ninajifunza mengi sana kupitia uchaguzi huu,nahisi Afrika ya kusini Ndio nchi pekee afrika yenye demokrasia ya kweli. Tumeshuhudia Mwaka huu kuwepo na ongezeko la vyama vingi vya siasa vikiwemo pia vya kidini kama vile vya kikristo na kiislam kitu ambacho kwa nchi yangu Tz hakipo. Uchaguzi Umeanza leo ambapo watu 800000 wenye mahitaji maalum watapiga kura na Siku ya Jumatano Utafanyika Rasmi uchaguzi huo wa serikali za mitaa ambapo zaidi ya Raia Milion 26 wanatarajiwa kupiga kura.