Uchaguzi wa rais mpya natamani ungekuwa kesho

AZUSA STREET

JF-Expert Member
Oct 31, 2013
2,007
1,894
Kulingana na fimbo zinavyopigwa, hakika uchaguzi ujao mambo yatakuwa tofauti na watu walivyotabiri mwanzoni mwa utawala huu. fimbo kwenye mishahara, fimbo pesa hamna kila eneo fimbo tu. dah...uchaguzi njoo haraka tafadhali
 
Hakuna mantiki hapo. Hujaelezea ni namna gani uchaguzi huo utaondoa hizo fimbo.
 
Bila shaka utakuwa miongoni mwa wagombea urais wakati ukifika
kwa hali ilivyo, hata kingwendu tu akigombea urais next election kuna uwezekano akapata kura nyingi sana. hali sio nzuri ati kwa watu wote, mafisadi na watu wema wote wanapata shida tu. ndio maana lema anamkumbuka msoga.
 
Kama uliishi kwa utapeli enzi hizo unategemea nini?
Tena upigwe tuu bakora kila siku
 
Kama uliishi kwa utapeli enzi hizo unategemea nini?
Tena upigwe tuu bakora kila siku
ajabu yake, mimi sipigwi kama wanavyopigwa watu wengine, au kama unavyopigwa wewe. namshukuru Mungu kwa hilo, na zaidi ya yote, sijawahi kuwa fisadi namtumikia Mungu. sema tu, nawaonea huruma watu mitaani wanavyohangaika kwa sasa. vilevile, tunamwombea kwa Mungu magufuli (kwasababu tumeshampata hatuna jinsi ya kumkataa hadi uchaguzi mwingine ndio kuna option hiyo kwa wale watakaotaka kumkataa), tumwombe kwa Mungu aili kila analofanya liwe na mkono wa Mungu kwasababu akifanya jambo ambalo halina mkono wa Mungu, inakuwa hasara.

najua anapata shida sana kwasababu ni sawa na wewe unakabidhiwa kampuni isiyo na hela na unatakiwa kuwalipa wafanyakazi uliowakuta mishahara, kwa kipindi cha muda fulani lazima mkubali kula mlenda ili mwakani mle kuku.
 
tuvumilie tu kuna wakati utafika mambo yatakuwa safi kuliko maelezo tutaenjoy sana kila mtanzania atapata furaha ya national cake
 
Back
Top Bottom