Uchaguzi wa marudio Zanzibar, Tunajitakia laana wenyewe

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,226
3,291
Kwamba dunia nzima haijui vigezo vya uchaguzi huru na haki na badala yake ZEC pekee ndio ina vigezo hivyo. Halafu wanakingiwa kifua na Serikali iliyomchaguwa mwenyekiti wake Jecha.

Kwamba uzoefu wa wazee wetu na wanadiplomasia hawajui athari za kususiwa na mataifa yenye nguvu kiasi cha kusubiri mpaka tuanze kuathirika watanzania wote kwa maslahi ya wahafidhina wachache na waroho wa madaraka.

Kwamba kwa makusudi tumeamua kubariki wazanzibari wabaguane na kurejesha uhasama wa asili na watu kufufukuzwa makazini na kubariki kuivuruga Katiba ya Zanzibar toleo la 2010.

Kwamba wasomi wote waliopo na wazoefu wa uongozi hawajui hatari iliyopo inayonyemelea Zanzibar. Wamenyamaza kimya wakumuacha mtawala (CCM) akifanya atakavyo kule Zanzibar na kwamba tumeshindwa kujuwa maana halisi ya Uzalendo, Usawa, Haki na Uadilifu pamoja na maana ya demokrasia katika vyama vingi?

Kwamba hatujuwi repacation ya kurejewa uchaguzi uliokwisha malizika na washindi kupatikana halafu tunajisahaulisha kwamba unarejewa tena kwa sababu Chama tawala kimeshindwa? hii Precedence ni mbaya sana na itakuwa imeasisi uduikteta wa KUDUMU kwa mtawala. iTAKUWA KUANZIA SASA iwe NEC au ZEC wakijisikia watafuta ucxhaguzi na itakuwa hakuna awzaye kuzuwiya.

Hivi hao waliotandika Demokrasia wako wapi? hawalijui hili? nini hatma ya Zanzibar na Tanzania kwa Kadhia hii.

Hivi kwa hili hatujitakii laana wenyewe au ndio mtawala ana dola na bunduki?
 
Watu wanaojitoa muhanga sasa hivi kwenye nchi za wenzetu hawakupata hiyo courage walipo lala na kuamka ila ni manyanyaso waliosababishiwa na serikali zao haki yao iliyokandamizwa kwa mda mrefu vikajichanganya vyote vikakua ndani roho zao zikakomaa na wakaona hakuna hata haja ya kuendelea kuishi tena wacha nife nao....
 
Mtasema yote lakini lazima urudiwe. Tume imepewa mamlaka hayo na hakuna wa kuiingilia. Unataka kuifurahisha dunia?
 
Watu wanaojitoa muhanga sasa hivi kwenye nchi za wenzetu hawakupata hiyo courage walipo lala na kuamka ila ni manyanyaso waliosababishiwa na serikali zao haki yao iliyokandamizwa kwa mda mrefu vikajichanganya vyote vikakua ndani roho zao zikakomaa na wakaona hakuna hata haja ya kuendelea kuishi tena wacha nife nao....
Jitoe mhanga na wewe ukione cha moto, Nani alimtuma Seif ajitangaze mshindi?
 
Kuna mdau mmoja humu nimeona amecoment sehemu kuwa ndani ya CCM hakuna mtu mzima kiakili bali kimaumbile,sasa hapo tafakari mleta uzi kama kuna atakaekuelewa.
 
Ukweli unauma japo mchungu kama shubiri.Ingekuwa CCM imeshinda hata kwa goli la Mkono kama huku Tanganyika wangetangaziana ushindi
Hii sinema ya Zanzibar ikishapita sijui mtaibuka na nini na kuifanya habari ya mjini.
 
Kuna mdau mmoja humu nimeona amecoment sehemu kuwa ndani ya CCM hakuna mtu mzima kiakili bali kimaumbile,sasa hapo tafakari mleta uzi kama kuna atakaekuelewa.
Wewe hauna tofauti na chizi anayejiona mzima na kuanza kuwaita wazima machizi. Kichwani wewe zilishapungua siku nyingi.
 
Kiboko yenu Jecha tu mmoja, mmebaki kuweweseka subirini tarehe 20 mnyolewa halafu muje na hizi tungo zenu za juma jogo fyuuuuuu.
 
Hii sinema ya Zanzibar ikishapita sijui mtaibuka na nini na kuifanya habari ya mjini.

Kama watanzania tunatakiwa kuamini katika haki ,usawa,upendo na kuamini kwamba kila mtanznaia anayohaki ya kuongoza mradi akidhi vigezo.

Kama watanzania tunatakiwa kujiona wote tuko sawa japo itikadi zetu ni tofauti.Tusiwe wanafiki kama wanasiasa wanachokiongea sicho wanachokitenda.

Kila siku tunawaona akina Magufuli na Shein wakiwatukana wapinzani lakini leo wanaenda mbali zaidi kuwaona na kuwatakia afya njema na kupromise kufoot bills zao.

Leo ndugu yangu bila kujijua unatengeneza uhasama na mtu ambaye kesho huwezi jua atakusaidiaje.

TataMadiba litendee haki jina.Mwenye jina alikuwa anatukuza Haki.Na ndiyo sababu aliwatukana Warundi.Leo unafanya kinyume na jina lake.Kaka sisi sote ni watanzania,tunahaki kuwa watanzania,kuishi,kutembea na kuongoza.
 
Kiboko yenu Jecha tu mmoja, mmebaki kuweweseka subirini tarehe 20 mnyolewa halafu muje na hizi tungo zenu za juma jogo fyuuuuuu.

Jecha ndiyo anayeweweseka jini la kupindua sheria linamsonga
 
Jipe moyo ila habari ndio iyo tukutane 20 March , btw vipi kuhusu Maalim Seif kuja na wale watu wa umoja wa kimataifa? teh teh ishi na wajinga upate kuneemeka au kwa msamiati mwengine wajinga ndo waliwao. Mujini hapa
 
Kama watanzania tunatakiwa kuamini katika haki ,usawa,upendo na kuamini kwamba kila mtanznaia anayohaki ya kuongoza mradi akidhi vigezo.

Kama watanzania tunatakiwa kujiona wote tuko sawa japo itikadi zetu ni tofauti.Tusiwe wanafiki kama wanasiasa wanachokiongea sicho wanachokitenda.

Kila siku tunawaona akina Magufuli na Shein wakiwatukana wapinzani lakini leo wanaenda mbali zaidi kuwaona na kuwatakia afya njema na kupromise kufoot bills zao.

Leo ndugu yangu bila kujijua unatengeneza uhasama na mtu ambaye kesho huwezi jua atakusaidiaje.

TataMadiba litendee haki jina.Mwenye jina alikuwa anatukuza Haki.Na ndiyo sababu aliwatukana Warundi.Leo unafanya kinyume na jina lake.Kaka sisi sote ni watanzania,tunahaki kuwa watanzania,kuishi,kutembea na kuongoza.

Nakushukuru kaka.

kuna watu wanaleta ukereketwa hapa. Hili suala la Zanzibar linatengeneza Precedence mpya na mbaya kwa siasa za Tanzania.

Yanayowakuta wenzetu si bahati mbaya katika nchi nyengine. Ikiwa kwa hili kuna watu wanaona ni kawada shauri yao. ndugu wamoja hawaelewani kuna taarifa zinafichwa fuatilieni yanayoendelea kule Pemba. Kuna sehemu watu wamesisiwa harusi na maziko, na juzi tu watu walisusiwa kuvuushwa katika kisiwa kimoja na sasa serikali inapeleka majeshi.

Uhasama umerudi kwa kasi na viongozi hawana habari wao wanalotaka ni kujihalalisha na kubaki madarakani kwa gharama yoyote.

Sasaq hivi hakuna mzunguko wa pesa, vitu bei iko juu, kuna joto la ukimya na shari iliyojificha, kuna jinamizi la Presha ya mataifa makubwa na vikwazo.

Haya kuna watu hawayafikirii wanaleta unafiki kisa wanalipwa kwa kukesha mitandandaoni.
 
Jipe moyo ila habari ndio iyo tukutane 20 March , btw vipi kuhusu Maalim Seif kuja na wale watu wa umoja wa kimataifa? teh teh ishi na wajinga upate kuneemeka au kwa msamiati mwengine wajinga ndo waliwao. Mujini hapa

Kama huyo Jecha angekuwa mwanaume kweli,asingeweka picha za akina Maalim,lakini sababu ya kukosa kile alichokitaka katafuta redio nyingine.

Pole unapoona watu wajinga angalia pande yako yawezekana uzima wako unategemea ujinga wa upande wa pili
 
Mimi huwa sio muongeaji sana nasubiria 20 nikapige kura nyie subirieni Seif atangazwe kwenye matangazo ya vifo.
 
Nakushukuru kaka.

kuna watu wanaleta ukereketwa hapa. Hili suala la Zanzibar linatengeneza Precedence mpya na mbaya kwa siasa za Tanzania.

Yanayowakuta wenzetu si bahati mbaya katika nchi nyengine. Ikiwa kwa hili kuna watu wanaona ni kawada shauri yao. ndugu wamoja hawaelewani kuna taarifa zinafichwa fuatilieni yanayoendelea kule Pemba. Kuna sehemu watu wamesisiwa harusi na maziko, na juzi tu watu walisusiwa kuvuushwa katika kisiwa kimoja na sasa serikali inapeleka majeshi.

Uhasama umerudi kwa kasi na viongozi hawana habari wao wanalotaka ni kujihalalisha na kubaki madarakani kwa gharama yoyote.

Sasaq hivi hakuna mzunguko wa pesa, vitu bei iko juu, kuna joto la ukimya na shari iliyojificha, kuna jinamizi la Presha ya mataifa makubwa na vikwazo.

Haya kuna watu hawayafikirii wanaleta unafiki kisa wanalipwa kwa kukesha mitandandaoni.

Naomba ni kusahhishe kidogo mie ni jinsia ya kike.

Pili tatizo la watanzania tumekubali kubebeshwa chuki ya viongozi.Sababu viongozi wanachukizwa na upinzani,ndiyo sababu wanawachukia wapinzani.

Ona hao viongozi walivyowanafiki,wakikubali ubaguzi uendelee Zanzibar,wanakubali ile club yao ya Kisonge iandike matusi na ubaguzi wote kwa wapinzani Shein anathubutu kutoka Zanzibar ati anaenda kumjulia hali Maalim,kama si unafiki ni nini??Kwanini watanzania hatulioni hilo??Kwanini hatusemi Hapana kwa ubaguzi huu,ni ajabu tunayapigia makofi maovu yanayofanywa na jeshi la polisi kwa wapinzani,halafu tunarudi nyuma kula matapishi yetu tukipiga makofi ati watawala wanawapenda wapinzani kisa ameenda kumuona mgonjwa.Unafiki huu hauhitajiki.
 
Mimi huwa sio muongeaji sana nasubiria 20 nikapige kura nyie subirieni Seif atangazwe kwenye matangazo ya vifo.

Utakufa wewe utamwacha Seifu.Acha Chuki na uhasama huyo Seifu ni Mtanzania kama alivyo Shein.Jifunzeni kumuogopa Mungu.Hata wewe huijui kesho yako.
 
Hamna mwenye chuki kufa ni kwa kila mwanadamu na Zanzibar mtu akifa anatangazwa kwenye ile radio adhim ZBC ili kila mtu amsikie , wewe subiria tu ata wewe unaweza kufa naona hujazingatia ilo.
 
Unapomuombea mwenzio kifo unadhani uko tofauti???Naona mlisheherekea kuona Maalim ameugua ghafla??ANgalieni msije mkaondoka nyie mkamuacha Mzee wa watu anapeta.

Ukitaka kujua kwa nini nimekujibu nilivyokujibu ni kwa sababu ya bandiko lako la kwanza.Ona aibu.
 
Back
Top Bottom