Zanzibar 2020 Zanzibar: Watendaji wa ZEC na Polisi kupiga kura Oktoba 27 badala ya Oktoba 28

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,036
2,000
Mwenyekiti wa ZEC jaji mstaafu Mahmoud ametangaza uchaguzi wa Zanzibar wa Rais, wawakilishi na madiwani kufanyika tarehe 27 na 28 Oktoba,2020.

Tarehe 27 Oktoba ni maalumu kwa watendaji wa tume, wajumbe wa tume na Polisi ambao watakuwa zamu siku ya tarehe ya uchaguzi.

Tarehe 28 itakuwa uchaguzi wa jumla

My take. Sasa ni rasmi kwamba demokrasia imechukuliwa. Tusubiri vurumai ya matokeo.

======

TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imetangaza Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa urais na uwakilishi utafanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa ZEC, Jaji Mkuu mstaafu, Hamid Mahmoud wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi tarehe 30 Julai 2020 visiwani humo.

Jaji Mahmoud amesema, kura ya mapema kwa watendaji wanaosimamia majukumu ya uchaguzi huo, itafanyika siku moja kabla yaani Jumanne tarehe 27 Oktoba 2020.
“Natangaza rasmi tarehe ya uchaguzi itakuwa Jumatano tarehe 28 Oktoba mwaka huu, ndugu wananchi, sheria ya uchaguzi imetoa nafasi kufanyika kura ya mapema, napenda kuwajulisha, upigaji kura ya mapema itafanyika tarehe 27 oktoba 2020 siku moja kabla ya upigaji kura pamoja,” amesema Jaji Mahmoud.

Mwenyekiti huyo wa ZEC amesema, kura ya mapema itahusisha wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wa vituo vya uchaguzi na askari polisi watakaokuwa zamu siku ya uchaguzi. Wajumbe na watendaji wa tume.

“Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, upigaji kura mapema utahusisha watendaji wanaosimamia majukumu ya uchaguzi siku ya uchaguzi, watendaji hao ni wasimamizi wa uchaguzi, wasaidizi wasimamizi uchaguzi, wasimamizi wa vituo, askari polisi watakaokuwa kazini siku ya uchaguzi ,” amesema Jaji Mahmoud.
Siku hiyo ya uchaguzi mkuu, inafanana na ile iliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania kuwa, uchaguzi mkuu utafanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

NEC ilisema shughuli ya uchukuaji fomu kwa wagombea ambapo wagombea wa ubunge na udiwani watachukua fomu tarehe 12 hadi 25 Agosti 2020, katika ofisi za NEC za halmashauri na kata nchi nzima.

Uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 25 Agosti 2020, huku kampeni zitaanza tarehe 26 Agosti hadi 27 Oktoba 2020.
 
GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
3,213
2,000
Mwenyekiti wa ZEC jaji mstaafu Mahmoud ametangaza uchaguzi wa Zanzibar wa Rais, wawakilishi na madiwani kufanyika tarehe 27 na 28 Oktoba,2020.

Tarehe 27 Oktoba ni maalumu kwa watendaji wa tume, wajumbe wa tume na Polisi ambao watakuwa zamu siku ya tarehe ya uchaguzi.

Tarehe 28 itakuwa uchaguzi wa jumla

My take. Sasa ni rasmi kwamba demokrasia imechukuliwa. Tusubiri vurumai ya matokeo.
Hata huku Bara polis watapiga kura Tar 27 halafu wananchi wa kawaida Tar 28
 
S.M.P2503

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
657
1,000
Kura mamluki zitajazwa kwenye hayo mabox ya tarehe 27
Idadi ya askari si inajulikana au ? hata jumla ya wanajeshi pia inajulikana... hawafiki Million in total maana budget hakuna ya kuwatosheleza.

Jeshi pekee Tanzania nzima (polisi na wanajeshi) :

sema kwa mfano kwa jeshi la polisi ni 5000 kila mkoa, zidisha kwa idadi ya mikoa, hawafiki hata nusu million.
na huko zanzibar ni pungufu pia, wote hawawezi kuwa ccm, labda Yesu aje...

kwa jeshi Tanzania:
Total Military Personnel
110,000 est; Active Personnel 30,000 est ;Reserve: 80,000...

hata kama jeshi zima likihamia zanzibar, kuchakachua kura zote ni mtihani. Ndio maana tunasema mambo yawe wazi na hukuna haja ya kutenga siku mbili kupiga kura.

source: 2020 Tanzania Military Strength
 
komanyahenry

JF-Expert Member
Sep 15, 2017
746
1,000
Hapo ni kwa ajili ya kujaza kula fake pamoja na kuwatisha askari kuchagua upinzani, jamaa alimaindi jimbo la kawe kuchukuliwa na upinzani ilihali asilimia kubwa ya wakazi wa kitongoji cha kawe ni wanajeshi
 
KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,036
2,000
Ilimradi uchaguzi wa wazi kabisa wa 2015 Jecha aliachwa kuufuta mbele ya dunia, hakuna kinachoshindikana tena sasa.
Mkakati use ni mbele kwa mbele tu.

Ngoja tuwasubiri wapinzani wa kweli na wale waunga juhudi na feki.
 
Gasy wa Ukweli

JF-Expert Member
Nov 7, 2010
377
250
Idadi ya askari si inajulikana au ? hata jumla ya wanajeshi pia inajulikana... hawafiki Million in total maana budget hakuna ya kuwatosheleza.

Jeshi pekee Tanzania nzima (polisi na wanajeshi) :

sema kwa mfano kwa jeshi la polisi ni 5000 kila mkoa, zidisha kwa idadi ya mikoa, hawafiki hata nusu million.
na huko zanzibar ni pungufu pia, wote hawawezi kuwa ccm, labda Yesu aje...

kwa jeshi Tanzania:
Total Military Personnel
110,000 est; Active Personnel 30,000 est ;Reserve: 80,000...

hata kama jeshi zima likihamia zanzibar, kuchakachua kura zote ni mtihani. Ndio maana tunasema mambo yawe wazi na hukuna haja ya kutenga siku mbili kupiga kura.

source: 2020 Tanzania Military Strength
Mkuu sasa hapa sanduku la kura halifunguliwi mpaka uchaguzi umalizike tar 28 so haitaweza kujua idadi ya kura za askari au wafanyakazi wa tume
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom