Uchaguzi wa Mameya Kinondoni na Temeke kurudiwa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,720
55,859
Habari wakuu,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), George Simbachawene, amesema kuwa kufuatia Rais Magufuli kuridhia kuundwa kwa Wilaya mpya baadhi zikiwa Jijini Dar, ambazo ni Wilaya ya Kigamboni na Ubungo, ni dhahiri baadhi ya Madiwani itabidi wakae kwenye Halmashauri zao ambazo zinaanzishwa ili wachague Mameya

Kuhusu uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar, alisema utakuwa Februari 8 mwaka huu.

Wilaya zilizoongezwa na Wilaya ya Kigamboni na Wilaya ya Ubungo, hivyo Madiwani nao wamegawanyika kutokana na Mgawanyo wa Wilaya.

Natumaini huu utakuwa mwisho wa hujuma katika Uchaguzi wa Mameya wa Dar es Salaam.
 
Gharama.....Gharama.....Gharama......Kata mti panda mti.Punguza huku ongeza kule.Hapa kazi tu hakuna kibarua.
 
Uchaguzi wa meya Kinondoni, Temeke kurudiwa

Uchaguzi wa mameya katika manispaa za Temeke na Kinondoni, Dar es Salaam utarudiwa katika kipindi kifupi kuanzisha sasa baada ya Serikali kutangaza wilaya sita mpya zikiwamo mbili za mkoa huo.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene alipokuwa akitangaza rasmi kuanzishwa kwa Mkoa wa Songwe unaomegwa kutoka Mbeya pamoja na wilaya hizo
CHANZO: MWANANCHI
 
Hembu waache kinondoni chini ya ukawa bwana! yaani shida yao waichukue kinondoni tu waendelee kuficha uchafu wao ulio kubuhu huko!
 
Naona hizo wilaya zimegawanywa kisiasa zaidi, kwani hata majimbo yaligawanywa kisiasa zaidi sio uhalisia wa mambo, lakini kumbuka siku ya kufa nyani miti yote huteleza.
 
Hakuna mwenye kutusaidia Analysis ya Mgawanyo wa Madiwani kutokana na ujio wa Wilaya hizi mbili za Kigamboni na Ubungo? Je,ipi ni impacts ya Ushindi uliokwishapatikana dhidi ya UKAWA?
 
Pombe naomba unajaribu kutafta ushindi ili kinondoni irudu lumumba ila mwisho utabaki kuumbuka epuka kutumia nguvu nyingi bila kufikiria maana inondoni chini ya ukawa unawauma sana. Endelea na ujecha wa nzanzibar
 
Uchaguzi wa mameya katika manispaa za Temeke na Kinondoni, Dar es Salaam utarudiwa katika kipindi kifupi kuanzisha sasa baada ya Serikali kutangaza wilaya sita mpya zikiwamo mbili za mkoa huo.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene alipokuwa akitangaza rasmi kuanzishwa kwa Mkoa wa Songwe unaomegwa kutoka Mbeya pamoja na wilaya hizo.

Chanzo:Mwananchi
 
Kuna watu huwa wanaichukulia poa ile TAWALA katika chama tawala.
 
Nadhani kinatafutwa kama kile cha Mwanza na Ilemela mwaka uleeeee
 
Kuna watu huwa wanaichukulia poa ile TAWALA katika chama tawala.
Ile TAWALA katika chama tawala inabeba ujumbe mzito sana, sasa ipo siku mkoa wa dar utakuwa na wilaya kumi... na wilaya moja itakuwa ukubwa usiozid kata nne
 
Narudia tena kuna siku nchi hii kila tarafa itakuwa wilaya na kila wilaya itakuwa mkoa kama iliyokuwa wilaya ya Mpanda kuwa mkoa wa Katavi!!!

Mzigo wote huu anabebeshwa mlala hoi maskini!!!
 
Back
Top Bottom