Uchaguzi wa CHADEMA mkoa wa Singida, ukabila watawala

Ndugu wana jamvi, naomba kufafanua kidogo kuhusu ukabila uliotajwa na mtoa maada, kwanza nakushukuru kwa kukiri mwanzoni wa post yako kwamba nilisimamia uchaguzi vizuri kwa kufuata katiba ya Chadema, katiba ndio msingi wa uchaguzi huo, na katiba hiyohiyo haina hata kipengele kimoja kinachosema watu wachaguliwe kwa uwiano wa makabila.... ni vyema kwanza ukajua kwamba kulikuwa na wagombea wangapi wa kinyiramba kwenye kinyang'anyiro hicho na baadae utuambie kwanini walikuwa wachache ukilinganisha na wanyaturu,, halafu sio kweli kwamba walioshinda ni wanyaturu peke yao... yupo mnyiramba Katibu bawacha, yupo mnyamwezi Mwenyekiti Bavicha ambaye alichuana na wanyiramba wawili, yupo mpare Mwenyekiti bawacha aliyewashinda wanyaturu wawili....nawashauri ndugu zangu wanajamvi, tuache kufukua ardhi kwa lengo la kutafuta sumu badala yake tusema ukweli kuhusu mambo halisi yalivyofanyika ili tusiiposhe jamii.

vipi kuhusu kauli mbiu za kinyaturu zilikuwepo?
 
Hebu chukua hii
Nafasi ya mwenyekiti mkoa ilikuwa na wagombea 2 tuu.Wote wanyaturu,mshindi kapata 81 kura na mshindwa kapata kura 2.
Hapo ukabila upo wapi? Huyu aliyeshindwa kiasi hiki huku akiwa mnyaturu,ina maana yeye hajui hicho kinyaturu?
Ndaa ya njou mna shida kweli
 
Chadema ni chama cha wanyaturu.
Duuuu,ugambani kazi kweli
 
Msonsa nae ni mnyaturu? Huyu alifanyiwa mizengwe mingi kwa kuwa ni mnyiramba.
 
Hamjui msemalo, kila siku mnasema CDM ya wachaga leo CDM wameongea kinyaturu mmegeuka kuwa cha wanyaturu,wakiongea kiswahili je? Naomba jibu.....
 
Jumbe tumekuelewa, na Mungu akubariki kwa kuusimamia uchaguzi kwa uadilifu. Watu kama ninyi ndiyo mnaotakiwa katika ujenzi wa Taifa, watu mnaosimamia haki kwa kufuata kanuni na sheria za Taasisi mnazozihudumia.

Ndugu wana jamvi, naomba kufafanua kidogo kuhusu ukabila uliotajwa na mtoa maada, kwanza nakushukuru kwa kukiri mwanzoni wa post yako kwamba nilisimamia uchaguzi vizuri kwa kufuata katiba ya Chadema, katiba ndio msingi wa uchaguzi huo, na katiba hiyohiyo haina hata kipengele kimoja kinachosema watu wachaguliwe kwa uwiano wa makabila.... ni vyema kwanza ukajua kwamba kulikuwa na wagombea wangapi wa kinyiramba kwenye kinyang'anyiro hicho na baadae utuambie kwanini walikuwa wachache ukilinganisha na wanyaturu,, halafu sio kweli kwamba walioshinda ni wanyaturu peke yao... yupo mnyiramba Katibu bawacha, yupo mnyamwezi Mwenyekiti Bavicha ambaye alichuana na wanyiramba wawili, yupo mpare Mwenyekiti bawacha aliyewashinda wanyaturu wawili....nawashauri ndugu zangu wanajamvi, tuache kufukua ardhi kwa lengo la kutafuta sumu badala yake tusema ukweli kuhusu mambo halisi yalivyofanyika ili tusiiposhe jamii.
 
Wanyiramba hawafai sio?Kumbe ndio maana mliwabagua.
 
Back
Top Bottom