Wadau jana CHADEMA mkoa wa singida walifanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wao,watakaodumu hadi 2019.
Kwa sehemu kubwa uchaguzi huo uliendeshwa kwa utulivu na umakini mkubwa chini ya msimamizi David Jumbe,ambaye wajumbe wengi wamempongeza kwa kuzingatia kanuni,miongozo na katiba ya CHADEMA.
Jumbe amejitofautisha kabisa na Shaban Limu aliesimamia chaguzi za majimbo na wilaya kwa kukiuka kanuni za uchaguzi kwa makusudi ili awapitishe wale ambao wangemuunga mkono.
Licha ya uchaguzi wa jana kwenda vizuri tatizo lililojitokeza ni ukabila wa wazi kabisa uliofanywa na baadhi ya wagombea,uliopelekea viongozi wote waliochaguliwa kuwa ni wanyaturu pekee.
Walijinadi kwa wapiga kura kwa lugha yao ya kinyaturu kana kwamba huo ulikuwa mkutano wa wanyaturu.
Tabia hii ya ukabila hasa kwa wanyaturu isipokemewa itazaa makundi yenye mirengo ya kikabila,jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wa demokrasia.

Ndugu wana jamvi, naomba kufafanua kidogo kuhusu ukabila uliotajwa na mtoa maada, kwanza nakushukuru kwa kukiri mwanzoni wa post yako kwamba nilisimamia uchaguzi vizuri kwa kufuata katiba ya Chadema, katiba ndio msingi wa uchaguzi huo, na katiba hiyohiyo haina hata kipengele kimoja kinachosema watu wachaguliwe kwa uwiano wa makabila.... ni vyema kwanza ukajua kwamba kulikuwa na wagombea wangapi wa kinyiramba kwenye kinyang'anyiro hicho na baadae utuambie kwanini walikuwa wachache ukilinganisha na wanyaturu,, halafu sio kweli kwamba walioshinda ni wanyaturu peke yao... yupo mnyiramba Katibu bawacha, yupo mnyamwezi Mwenyekiti Bavicha ambaye alichuana na wanyiramba wawili, yupo mpare Mwenyekiti bawacha aliyewashinda wanyaturu wawili....nawashauri ndugu zangu wanajamvi, tuache kufukua ardhi kwa lengo la kutafuta sumu badala yake tusema ukweli kuhusu mambo halisi yalivyofanyika ili tusiipotoshe jamii.