ALWATAN KIZIGO
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 539
- 642
Siku ya tarehe 28/3 2017 nilipost ujumbe mfupi kwamba Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amefanya uhuni na udikteta kwa kulazimisha kupitisha jina la Bwana Philimon Ndesamburo kua mgombea pekee katika nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Kaskazini katika uchaguzi uliotarajiwa kufanyika siku ya jana tarehe 29/3/2017.
Philemom Ndesamburo alikua anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Bwana Daniel Ole Porokwa ambaye aliondolewa katika kinyanga'nyiro hicho kimabavu kwa amri ya Mwenyekiti Mbowe.
Sasa kitendo hicho kilisababisha vurugu kubwa baina ya wajumbe wa kamati kuu na wengine wakasusia kikao na kurudi Dar baada ya kutoridhishwa na hatua ya Freeman Mbowe kuwaburuza kwa kulazimisha kulipitisha jina alilokuja nalo mfukoni la Philemon Ndesamburo .
Jana tarehe 29/3/2017 ni siku ambayo ilipangwa kufanyika uchaguzi huo na ulipangwa kufanyika katila Hotel ya Regal Naivera jijini Tanga .
Kulingana na taarifa zilizopatikana shughuli hiyo ya uchaguzi ilipangwa na Freeman Mbowe ilikua ianze majira ya saa nne kamili asubuhi, ambapo wanachama wa CHADEMA kutoka katika viunga mbali mbali vya jijini Tanga walianza kujikusanya katika Hotel hiyo ya Regal Naivera kuanzia saa moja asubuhi.
Lakini kwa masikitiko makubwa ilipofika saa nne,hakukua na kiongozi yeyote wa CHADEMA aliyekuja.Wajumbe waliendelea kusubiri huku wakiwa hawajakunywa chai wala maji ya kunywa mpaka saa 11 na nusu jioni ndipo Mbowe akiwa na baadhi ya viongozi wenzake na mgombea wake Philemon Ndesamburo, wakafika na kukuta wajumbe wakiwa taabani kwa njaa na kiu ya maji.
Baada ya kufika haraka haraka wakaingia ukumbini na wakawatangazia wajumbe wa uchaguzi huo kwamba, wamebadilisha agenda ya kufanya uchaguzi katika mkutano huo na hivyo mkutano huo utakua ni wa kawaida bila ya kufanyika uchaguzi .
Hatua hiyo ilisabaisha zogo kubwa ukumbini hapo,baadhi ya wajumbe wakamuomba Mwenyekiti awaonee huruma kwa kuwanunulia chakula , lakini Mbowe akawajibu kwa dharau kwamba hawajaja hapo ukumbini kuwalisha watu wazima chakula cha bure na hata hivyo hotelini hapo kuna chakula kinauzwa hivyo kama mtu ana hela aende akajinunulie.
Baada ya kutoa kauli hiyo wajumbe wengi wenyeji wa Tanga waliondoka ukumbini hapo na kumuacha Mbowe akihutubia wajumbe aliokuja nap kutoka Dar es Salaam na mikoa mingine.
Taarifa za ndani zinasema sababu ya kutokufanyika uchaguzi huo ni wajumbe wengi wa kamati kuu walikua wamekasirishwa sana kutokana na hatua ya Mbowe kulazimisha swahiba wake Philemon Ndesamburo apite bila kupingwa kwa kumuondoa Daniel Ole Porokwa kinyemela kuwania nafasi hiyo.
Ikumbukwe kwamba Freeman Mbowe alifikia katika Hotel ya Mkonge Hotel ambako siku ya tarehe 28/3/2017 walifanyia kikao cha kamati kuu katika ukumbi wa Hotel hiyo ambapo gharama za kukodi ukumbi hapo Hotelini ni shillingi million 5 za kitanzania ambapo jumla walitumia shillingi million 10 kwa sababu waliutumia ukumbi huo kwa siku mbili .
Na gharama walizotumia kukodi ukumbi katika Hotel ya Regal Naivera ni shillingi milioni 6 haikueleweka sababu zilizopelekea Mbowe kuamua kutumia ukumbi wa Regal Naivera ambao gharama zake ni kubwa kulinganisha na Mkonge Hotel.
Jumla ya bajeti kuu ambayo CHADEMA waliipanga kufanikisha uchaguzi huo ni shillingi Milion 75 lakini kutokana na uhuni wa Mwenyekiti Mbowe uchaguzi huo haukufanyika na pesa shillingi Milion 75 za ruzuku zikapotea bure.
Huu ni muendelezo wa jinsi Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe anavyotumia vibaya ruzuku za chama hicho kujinufaisha yeye binafsi na watu wake wa karibu.