Uchaguzi UWT vituko vitupu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi UWT vituko vitupu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIGENE, Oct 11, 2012.

 1. KIGENE

  KIGENE JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,068
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  WAKATI uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) ya CCM ukikaribia, wagombea nafasi ya uenyekiti wamezidi kutuhumiana kwa matumizi makubwa ya fedha, huku mmoja wao akidai kujinadi kwa kutumia jina la Rais Jakaya Kikwete.

  Taarifa zinaeleza kuwa wagombea watatu waliopitishwa majina yao na Kamati Kuu ya CCM kuchuana katika kiti cha UWT Taifa ni Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Sophia Simba, Anne Kilango na Maryrose Majige.
  Wakati mchuano mkali ukionekana kuwa baina ya Simba ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na Mbunge wa Same Mashariki, Kilango, bado Majige naye anapewa nafasi kubwa kutokana na mtandao wake ndani ya chama.

  Wakati akichukua fomu za kutetea kiti hicho mjini Dodoma, Waziri Simba bila kutaja jina, alidai mpinzani wake mmoja ameanza kugawa fedha mikoani kwa kuwatumia wanaume ili kuwashawishi wajumbe wampigie kura. Simba ambaye amekuwa kwenye msuguano wa kisiasa na rafiki yake Kilango, alitamba kuwa pamoja na mpinzani wake kucheza rafu hiyo na kumtumia vitisho vya kumtaka asigombee, yeye anajivunia mtaji wa utendaji mzuri katika jumuiya hiyo.

  Hata hivyo, Kilango naye alijibu mapigo akidai kuwa amejitosa kuwania uenyekiti wa UWT ili kukiokoa chama kutokana na fukuto kali la upinzani linaloshika kasi.
  Kilango bila kumtaja jina la mpinzani wake, aliipinga waziwazi sera yake ya kutaka viti maalumu viwekewe ukomo wa awamu mbili.

  Huku hali ikiwa hivyo, Tanzania Daima imedokezwa kuwa mmoja wa wagombea hao watatu, ameanza kujinadi kwa wapigakura kwa kutumia jina la Rais Kikwete akidai ametumwa agombee ili kukiimarisha chama kinapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

  Mgombea huyo ambaye jila lake tunalihifadhi kwa sasa, pia anadaiwa kupita kwa baadhi ya wakurugenzi wa taasisi za umma na wafanyabiashara maarufu nchini kuomba fedha zitakazomsaidia kufanikisha kampeni yake ya kunyakua kiti hicho.

  Mmoja wa wafanyabiashara waliofikiwa na mgombea huyo amelieleza gazeti hili kuwa, alimweleza kwamba anahitaji msaada wa fedha kwa ajili ya kampeni zake na kwamba iwapo atamsaidia, atakuwa amemsaidia rais kwa sababu anamuunga mkono. Alisema alitilia shaka maelezo hayo kwa sababu ya kutambua misimamo ya mgombea huyo na kuamini kuwa huenda alifika pale kumtega kwa sababu CCM sasa inapambana na rushwa.

  Mfanyabiashara huyo aliongeza kuwa, baada ya mgombea huyo kumuhakikishia kuwa hakuwa na nia mbaya, alikuwa tayari kumsaidia lakini alishindwa kutokana na kiwango kikubwa alichokiomba.

  Mmoja wa wenyeviti wa UWT mkoani Pwani, naye aliliambia gazeti hili kuwa mgombea huyo amekuwa akitumia fedha nyingi kuwapigania baadhi ya wagombea walio katika kambi yake ili washinde na kwenda kumpigia kura taifani.
  Mgombea huyo anadaiwa kuwa ameanza kupita kwa wajumbe akiwadanganya kuwa Rais Kikwete amemtuma awanie wadhifa huo na kwamba yuko nyuma yake.

  "Huu uchaguzi usipoangaliwa utakuwa uchaguzi uliojaa uchafu kuliko chaguzi zote. Hawa wanaowania uenyekiti wa UWT, wapo ambao wameanza kutumia jina la rais kuwadanganya wapiga kura kuwa amewatuma wagombee na atahakikisha anawasaidia kushinda," kilisema chanzo chetu.

  Kwamba wakati mwingine baadhi ya wajumbe wamekuwa wakimwamini mgombea huyo kwa sababu akiwa nao ananyanyua simu na kuwapigia watu wake kwenye sekretariati na kuzungumza nao kuhusu mwenendo wa kampeni zake hadi kufikia hata kutishia kuwafukuza baadhi ya viongozi wa wilaya.

  "Sisi tunaamini rais hana mtu na akijua nadhani atakasirika sana kwa sababu jina lake linachafuliwa kutokana na uroho wa watu kutaka madaraka. Haiwezekani mtu anakwenda kwa wakubwa wa mashirika ya umma na taasisi anawaomba fedha kwa jina la rais," alisema.

  Kwamba kwa kutuma jina la rais amefanikiwa kuwanasa hata mahasimu wake wa kisiasa ambapo kuna mmoja aliwahi kupigana naye ofisini akiwa Katibu wa Wilaya wa chama na walikuwa katika uhusiano mbaya, lakini sasa ndiye mpiga debe wake mkubwa.

  Licha ya vikao vya juu kupiga marufuku kampeni za kuwafuata wajumbe, mgombea mwingine anadaiwa kufanya kampeni kali ya mkoa kwa mkoa ambapo wiki iliyopita alikamilisha kampeni zake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na sasa yuko mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
  Source : Tanzania Daima
   
 2. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Tuwaache wafu wazike wafu wao....
   
 3. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Source: tanzania daima GAZETI LA UENEZI CDM
   
 4. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hao ni wake za wakubwa wa magamba; isingekuwa hivyo wangefutiliwa mbali majina yao kwa kukiaibisha chama chao kwa matusi wanayotupiana!!
   
Loading...