Uchaguzi UVCCM..Ally Hep Vs Sango: Mapandikizi ya Ridhiwani na Saanane | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi UVCCM..Ally Hep Vs Sango: Mapandikizi ya Ridhiwani na Saanane

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ben Saanane, Aug 3, 2012.

 1. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Hayo ya Ben Saanane kupandikiza ni uongo


  ''uchaguzi wa uvccm umeanza kwa kuingiliwa na vyama nje ya ccm huku baadhi ya wanasiasa nje ya umoja wa vijana kupanga safu yao.ridhiwani anatuhumiwa kumpandikiza ally hepi aliyekuwa kiongozi wa DARUSO huku baadhi ya wanasiasa vijana nje ya CCM wakipandikiza wagombea wao kwa ustadi ndani ya jumuiya.Maandalizi ya kuchukua fomu hadi uandishi wa matamko yao na hata ufadhili unafanywa na baadhi ya watu kwa maslahi ambayo hayaendani na umoja wa vijana.
  Hali hii inatishia uchaguzi huru na wa hakli kwa maslai ya baraza la vijana kwani madhumuni ya mipango hii hayajawekwa wazi.siasa za kuchafuana zinasukwa kwa ustadi mkubwa unaohusisha mbinu za kimafya jambo ambalo linakosesha haki kwa watoto wa wakulima wasio na watu wa kuwapigia vifua.hali ya mgawanyiko ndani ya chama ndiyo inayoendelea kukiumiza chama jambo lililotoa mwanya kwa vyama vya upinzani kujipenyeza na kuunga mkono baadhi ya wagombea kwa maslahi binafsi.''
   
 2. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,897
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  Good news better yet who cares
   
 3. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #3
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  I think you should clap for yourself. However popular those words are. Those who uses them are silly and uncultured.Allegations without envidence!

  To be candid with you,stop making silly political excuses.

  Sina haja ya kupandikiza mtu UVCCM.Siwezi kumuondolea mashine ya oksijeni mgonjwa aliyeko ICU.Chama chenyewe kimeshakufa nijishughulishe nacho kwa nini.Naomba msinihusishe na hizo siasa zenu.Sipendi ujinga huu mnaofanya.Endeleeni kuchafuana huko vichochoroni
   
 4. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Who cares?
   
 5. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  kamanda Ben just ignore those guys who think by simple mind and spends 24 hrs 4 discusing people instead of logic.
  Bali endeleza mapambano kukijenga chama (CHADEMA) kama sisi kesho hapa moro tutakuwa na M4C.

  FEAR NOT.
   
 6. Young Tanzanian

  Young Tanzanian JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,740
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  duh baada ya puma wamehamia uvvcm...kila ktu kina mwsho hatupo mbali hii ni mikakat ya urais 2015 bt watafel
   
 7. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Nilikuwa nakusubiri. Umejibu vizuri ila hapo kwenye red ndio jibu la msingi!
   
 8. D

  Daniel Muhina Member

  #8
  Aug 3, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hey Guys! waacheni uvccm wafanye chaguzi zao kwa salama na amani, kwani chaguzi zote lazima ziwe na kelele za hapa na pale but long at last uchaguzi utafanyika kwa amani, na hakuna mtu mwenye kuweza kupanga safu kwakushawishi Tanzania nzima eti imchague fulani, ni kweli baadhi ya watu waweza kuwa na mchaguo yao lakini itategemea hayo machaguo yana kubalika vipi kitaifa! so if its Ally, Sango and who ever wapiga kura wataamua
   
 9. PPM

  PPM JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 839
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu mbona umelipuka kama mjamzito?
   
 10. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  moja kati ya coment za kijinga kabisa kukutana nazo hapa jukwaani. Very low!
   
 11. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  fanya sala ya kuomba hekima na busara
   
 12. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #12
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  tamko la sango
  PRESS STATEMENT

  HOTUBAYA MGOMBEA NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA (UVCCM) TAIFA- SANGOGUNGU KASERA

  2August 20112

  Ndg:Wanahabari
  Ndg: wanaUVCCM wenzangu

  Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa naomba kutoa salamu zangu za dhati kwa Watanzania na vijana wenzangu wanchi hii pamoja nanyi waandishi wa Habari kwa kushiriki nami katika safari hiiinayolenga kuunganisha na kujenga hatua za mabadiliko ya maisha ya Vijana waTanzania. Kwa namna ya pekee kabisa niwashukuru na kuwaomba mshikamano vijanawenzangu wa Chama cha Mapinduzi ambao kupitia kwao ninatumia nafasi hii kuomba ridhaa yao ili nipate nafasi ya kuwa chemchem ya mafanikio na mabadiliko katika maisha yetu kwa kuanzia na chama chetu. Leo hii naungana na vijana wenzangu hawa wa ndani ya CCM, kufanya jambo moja kubwa, jambo la kuchukua fomuya kuwania moja ya nafasi kubwa katika jumuiya ya Vijana wa CCM Tanzania. Ninafanya kazi hii leo nikitambua mambo yafuatayo:

  Kwanza, ninalenga kuleta mabadiliko yanayotazama aina ya vijana tuliopo sasa, aina ya maisha tunayoishi na aina ya changanoto zinazotukabili mimi nikiwa mmojawapo.

  Pili kwa upekee mkubwa, nachukua fomu hii nikibaini hali ya vijana huko tulikotoka na , changamoto tulizopitia na hatari inayotukabili mbele kama hatua stahiki hazitaanza kuchukuliwa na vijana wa aina yangu ambao tuna uzoefu wa kutosha wa maisha ya kawaida ambayo yanahitaji nguvu na akili zetu na za wenzetu waliotutangulia katika kuboresha maisha yetu ili tuweze kuwa raia wema katika nchi yetu na wanachama waadilifu wa chama chetu na jumuiya zake.

  Ndugu Waandishi wa Habari;

  Kazi hii ya kuchukua fomu ninayoifanya leo hii na kisha kuanza zoezi la kutafuta kuungwa mkono. Ni kazi inayohitaji ushirikiano mkubwa kwa uongozi wa Jumuiya yetu pamoja na vijana mbalimbali bila kujali itikadi zao za vyama vya siasa. Nasema hivi kwa kutambua kuwa UVCCM ndiyo Jumuiya pekee yenye kubeba taswira na matarajio ya vijana wa Tanzania na ambayo siku zote inatakiwa kusimamia maslahi na matakwa ya vijana wa Tanzania na kwakuwa jumuhia hii ni jumuhia ya chama kinachoongoza si chama tawala .

  Ndugu zangu wanahabari na wana CCM tunafahamu tofauti kati ya kuongoza na kutawala ndio maana nimetumia neno kuongoza, na Kama kazi hii ilikuwa haifanyiki huko nyuma na kama ilifanyika bila kuridhisha, mimi nimeamua kwa moyo mkunjufu kuingia kuonesha namna jumuiya yetu itakavyoweza kuwatumikia vijana wa Tanzaniana kukiboresha chama cha Mapinduzi ili kitambue wajibu wake kwa vijana wote waTanzania na kwa kufanya hivi kiweze kusimamia misingi iliyolijenga Taifa hili na kuachwa na waasisi wa Taifa letu Hayati Baba Wa Taifa na Hayati Rais Karume ambao walilijenga taifa letu katika misingi ya haki, usawa na ustahimilivu.

  Ndugu wana habari; Katika kipindi hiki chakutafuta nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea wa nafasi hii nitabakia kuongozwa na Moto isemayo: Vijana kwanza kwa taifa lenye amani na maendeleo. Bila vijana kuangaliwa na kupewa yale wanayostahiki, ni wazi taifa lenye amani na maendeleo halitakuwepo. Natambua fika kuwa vijana wa Tanzania wanakabiliwa na changamoto kubwa hasa ile inayolenga kubaini ndoto ya maisha yao ya sasa na siku zijazo. Naamini mimi ni mmoja wa vijana hawa ambaye pia ninahitaji kuona vijana walio katika kilimo basi wanaweza kupata soko la mazao yao. Vijanawabeba mikokoteni nao wanafanya kazi hiyo kwa miaka kadhaa na kisha kuboreshaajira zao.

  Vijana wanaosoma basi wanahitimu vema na kupata ajira wanazostahiki na pia walio makazini na waliopata nafasi za kuongoza wanaonesha mfano wakufanya kazi kwa kujituma na kwa bidii ili kuonesha kuwa vijana tunaweza na hatuwezi kuliangusha taifa. Natambua haya ninayoyazungumza ni mambo magumu lakini pia natambua yanahitaji mbinu nyingi ili kukabiliana nayo. Kwa sasa natumia nafasi hii kukiomba Chama changu, kuiomba Jumuiya Yetu ya Vijana kutambua kuwa nina dhamira, nina nia, nina sifa za kutosha, nina uwezo wa kufanya majukumu haya ninayoyaomba na ninafahamu kazi za majukumu haya.

  Tena nina rekodi katika umri wangu huu wa kufanya mambo ya kutukuka ambayo rekodi yake inaweza kutazamwa pote nilipobahatika kutoa utumishi wangu. Kwa namna isiyoonyesha kuyumba naomba kuwaeleza vijana wenzangu kuwa kutokanana mshikamano wa vijana wenzangu kwangu ni wazi tumejiandaa kushinda katika nafasi hii ili tuweze kuleta mwanga wa mabadiliko katika jumuiya yetu na chama chetu katika maandalizi ya chaguzi zijazo. Ndugu wanahabari ninatambua zipo changamoto nyingi zinazoikabili UVCCM na changamoto hizi zinahitaji kiongozi ambaye atakuwa na uthubutu wakuweza kukabiliana nazo, changamoto kuuni kitaswira, kimuundo, kiimani, kimadhumuni kama ambavyo zimehainishwa kwenyekanuni za ummoja wa vijana. Nina maanisha nini ninapozungumzia taswira ya UVCCM.Taswira ya UVCCM Taifa leo siotaswira ya kimapambano.

  Historia yetu ipo wazi jumuiya ya vijana ilishiriki katika mapambano ya kuleta Uhuru, Umoja na mshikamano mtakumbuka wakati TANU Inahangaika na kutafuta Uhuru wa Tanganyika na Afro-Shirazi party ikipambana kuleta Uhuru wa Zanzibar vijana waliunganishwa na jumuiya za umoja wa vijana wa vyama hivi viwili ambavyo ni TANU YOUTH LEAGUE na ASP YOUTH LEAGUE, zinafahamika kazi zilizofanywa na wabeba mizigo wa Kariakoo mfano Mzee Rajabu Diwani, leo UVCCM sio tena yawabeba mizigo, sio tena ya wamachingasio tena ya wakulima ,sio tena jumuiya ya wafanyakazi ni jumuiya ya wafanyabiashara, watoto wa vigogo ama wenyenasaba nao ama rafiki zao, inahitaji viongozi wenye dhamira ya dhati ambao watarudisha jumuiya hii kwa vijana wakitanzania na kurudisha taswira ya kimapambano ambayo ni mapambano ya kiuchumi, kazi ya Uhuru imeshafanyika imebakia jukumu la kuleta Uhuru wa kiuchumi na kuwa kimbilio la vijana wote.

  Ni dhamirayangu ya kugombea nafasi hii ni kuhakikisha awamu ya pili ya mapambano ya kiuchumi ya umoja wa vijana inaanza rasmi. Nafahamu zipo changamoto za kiutawala, kiuchumi na jumuiya kuendelea kuishi kwa kutegemea misaada na Ruzuku kutoka kwenye chama, nafahamu watendajiwana hali mbaya kiuchumi hasa katika mawilaya, nafahamu ofisi zetu za wilaya zina upungufu wa vitendea kazi ni dhamira yangu kubadili mwelekeo wa utendajiwa jumuiya yetu kutoka "Business as usual" kuvalisha skafu viongozi na kuimba nyimbo, kuwa jumuiya yenye dira namwelekeo sahihi wa kuwaunganisha na kumkomboa kijana wa kitanzania.

  Ndugu waandishi wa Habari; Ninafahamu matarajio yavijana wa kitanzania yatafikiwa kupitia CCM imara na CCM inatokana na uimara wajumuiya zake kuwa imara na hili inawezekana kwa kupatikana viongozi Imara na mimi nina amini ni mmoja waviongozi ambao wataifanya jumuiya yetu kuwa Imara.

  Kwa kuhitimisha Hotuba yangu naomba kutoa shukrani zangu kwa Mwenyezi Mungu kwa kunifanikisha kuwananyi hapa, niwashukuru wana familia yangu, marafiki na nyie ndugu zanguwaandishi wa Habari kwa kukubali kujumuika nami kunisikiliza leo. Niwaombe Vijana wenzangu wa CCM kuniunga mkono katika azma hii kubwa niliyo nayo na niwakumbushe tu kuwa, zoezi hili la kuchukua fomu nililofanya hapa leo si langu bali la vijana wote wa Tanzania wakiwakilishwa na Vijana wa Chama cha Mapinduzi.

  Ni imani yangu kuwa, wana UVCCM hawatakubali kuangusha taa hiiwaliyoiwasha kule Rorya mkoa wa Mara wao wenyewe na badala yake wataungana namibega kwa bega ili kuufikia ushindi. Tutapitisha fomu hii pamoja nao, tutachujwa pamoja nao na kisha tutashinda pamoja nao na kisha kuanza kuwaongoza vijana wa Tanzania pamoja nao. Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma atubariki na kutupa nguvutufanikishe azma hii muhimu pamoja. Kidumu Chama cha Mapinduzi

  Asanteni kwa kunisikiliza.

  Mimi Ndg Sango Gungu Kasera- Mjumbe Mkutano Mkuu UVCCM (W) Rorya

  Kauli mbiu Mbiu "Vijana kwanza kwa taifa lenye amani namaendeleo''.
   
 13. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #13
  Aug 3, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  salum hepi hajawahi kuwa kiongozi wa daruso tuacheni uwongo wa kumpandisha chati, nafkiri tumpeni nafasi atupe majibu kuhusu ela alizokuwa anapewa na mkandala ili afanye usaliti kwa wanafunzi kuhusu migomo iliyokuwa na maslahi kwa watoto wa masikini..ebu vijana tuwe realistic kidogo hivi huyu kidudu mtu riz one atatutawala mpaka lini, baba yake kashindwa yeye ana jipya gani? the best way ampeleke hepi akawe makamu WAMA.
   
 14. mndwadage

  mndwadage JF-Expert Member

  #14
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 345
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ficha upumbavu wako.!!!!
   
 15. Captain Phillip

  Captain Phillip JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 900
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Eti na wewe ni Great Thinker!!!What a ****
   
 16. PPM

  PPM JF-Expert Member

  #16
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 839
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mtaniuwa washikaji, mtu wa chadema asiguswe humu ndani?
   
 17. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  keshasahau kama yeye mwenyewe ni matokeo ya uja uzito.
   
 18. t

  thatha JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  haya ni majungu tu baada ya kujitathmini9 na kuona uwezo wako ni mdogo unaanza kuwachafua wenzako.
   
 19. t

  thatha JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  huku ni kumanga manga.kama umejiona kuwa huna uwezo kaa pembeni acha kuwachafua wenzako,sio vizuri
   
 20. B

  BUBERWA D. JF-Expert Member

  #20
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 446
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  ben! Bado tu unarumbana na brains ndogo kama hizi!
   
Loading...