Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 36,357
- 23,760
Ndugu zangu Watanzania,
Napenda kuwaambieni ya Kuwa Uchaguzi utafanyika katika mazingira ya amani ,utulivu na usalama wa kutosha kabisa pasipo bughudha wala vurugu ya aina yoyote ile kutokea. Lakini pia Mama yetu Mpendwa ndiye atakaye shinda kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima katika uchaguzi huo .
Na kwa ushindi huo wa kishindo ndiye atakaye apishwa kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili. Na ataongoza Taifa letu katika hali na mazingira ya Amani na utulivu mkubwa sana .huku Taifa likitamalaki na kuimarika kwa umoja , upendo na mshikamano wa watanzania wote.
Hii ni kwa kuwa watanzania wana imani kubwa na Mama. Wanamkubali ,kumpenda na Kumuamini sana juu ya uwezo wake wa kuweza kuwaongoza na kuwavusha katika nyakati zote ngumu na za majaribu pamoja na kuwaletea maendeleo na kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.
Watanzania wana imani Kubwa juu ya Maono aliyonayo Mama katika kulipeleka mbele Taifa letu kimaendeleo na maendeleo ya mtu mmoja mmoja. Hakuna mtanzania mwenye shaka wala wasiwasi wala hofu juu ya uimara ,uhodari , ushupavu na umadhubuti wa kiongozi alionao Rais wetu.
Watanzania wanakumbuka mazingira magumu aliyopokea Nchi RAIS wetu na namna alivyo onyesha uhodari katika kulivusha Taifa letu kuishinda mitihani iliyojitokeza mbele yetu kama Taifa. Ndio sababu watu wanamiminika na kufurika katika mikutano yake kumsikiliza.
Vijana wameona tumaini wakati wa Mama kwa ni wakati wake vijana wengi sana wamepata ajira za moja kwa moja serikalini na wengine kupitia secta binafsi. Ni wakati wa mama ambapo watumishi wa umma wamepata tabasamu na matumaini baada ya kupandishiwa mishahara yao,kupewa nyongeza ya kila mwaka ,kulipwa malimbikizo ya madeni yao ,kupandishwa madaraja mseleleko na kulipwa stahiki zao na marupurupu mengine kibao.
Ni wakati wa Mama ambapo wakulima wamejawa na furaha tupu baada ya Mama ndani ya muda mfupi wa uongozi wake kutoa ruzuku ya takribani Billion 726 wastani wa Billion 152 kila mwaka. Ni wakati wa Mama biashara zimeshamiri na mzunguko wa pesa mitaani kuongezeka. Hapo bado sijazungumzia ujenzi na usambazaji wa huduma za kijamii karibu kabisa na mwananchi. Elimu bure hadi kidato cha sita na mengine mengi sana.
Ndio sababu watanzania wanasema Mama ANATOSHA na anastahili kupewa Mitano tena kuendelea kuliongoza Taifa letu.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.