Amma kwa haki wewe ujinga ni wa asili. Inflation unajuwa maana yake lakini au unajisemea tu? Kuna wakati Tanzania hii ambapo inflation rate ni ndogo na stable ya huu wa Kikwete? unataka nianze kukumwagia data hapa?
Tanzania kwa sasa siyo kukopesheka tu na kuthaminika vile vile wakati huu wa Kikwete ndiyo umeanza kuthaminiwa kama Mtanzania. Una Gas cubic feet trillion 55 na bado uchunguzi aliouanzisha Kikwete haujaisha. Kumbuka hilo.
Nyerere alipopewa hii nchi ilikuwa ya kwanza katika ku export mazao ya shambani, miaka saba baadae akatufanya kuwa omba omba wa kwanza duniani, njaa mtindo mmoja na mpaka anang'atuka miaka 24 baadae bado katuacha masikini wa mwisho duniani, umri wa kuishi Mtanzania aliouacha Nyerere haukufika hata miaka 39, hayajuwi hayo?
Leo unajuwa nani kakupandisha na unategemewa kuishi miaka mingapi ukizaliwa? Nani katupandisha chati? Si Mwinyi, si Mkapa, ni Kikwete katika kila nyanja, hata hii demokrasia tuliyonayo leo tunayoringia ni matunda ya nani zaidi ya Kikwete. Ulikuwa unaweza kufunguwa mdomo wako wakati wa Nyerere, Mwinyi au Mkapa? Thubutu!