Wakuu,
Baada ya kushuhudia matukio ya wiki chache zilizopita kama vile Mrema wa TLP kuhudhuria mkutano wa CCM an CHADEMA kupokea kwa mikono miwili msaada wa fedha kutoka kwa mfanyabiashara Sabodo ambaye ni mwanachama "damu" wa CCM, nimegundua kwamba vyama vyetu vya siasa ni usanii mtupu.
Pia hizi chaguzi zetu ambazo chama tawala kinatangaza uhakika wa kushinda miaka kabla ya uchaguzi wenyewe na kila mtu kuitikia wito naona ni jambo la mzaha.
Mimi napendekeza katiba ibadilishwe kufuta chaguzi na vyama vya siasa vyote hapa nchini. Badala yake tuwe na utawala wa kifalme na mfalme au malikia atakayetawala maisha na atakua anateua wasaidizi wake kutawala majimbo.
Tukifanya hivi kwanza tutaokoa matrilioni ya fedha zinazopotea katika kugharimia chaguzi na kuvilipa vyama vya siasa ruzuku. Hizi badala yake zitawekezwa kwenye sekta muhimu kama elimu, afya, nishati na miundombinu.
Pili, uchumi utakua kwa kasi ya ajabu kwasababu wale watu wote waliokua wanajihusisha na malumbano yasiyokua na tija chini ya kivuli cha siasa sasa wataelekeza nguvu na maarifa yao kwenye shughuli nyingine za ujenzi wa taifa kama vile uhandisi, utabibu, ualimu, biashara na michezo.
Ikiwa huu utawala wa kifalme utashindwa kusimamia maendeleo yetu na kukidhi mahitaji yetu kiasi cha kuamsha hasira na hisia kali ndani yetu sisi wananchi wa kawaida, basi tutaupindua na hapo ndipo DEMOKRASIA YA KWELI itakapozaliwa.
N