Uchaguzi Tz ni kuchezea fedha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi Tz ni kuchezea fedha

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Jumboplate, Jul 12, 2010.

 1. Jumboplate

  Jumboplate Senior Member

  #1
  Jul 12, 2010
  Joined: Jul 29, 2008
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimekuwa nikifuatilia sana vipindi (miaka) ya chaguzi na kugundua kuwa fedha nyingi sana hapa Tanzania zinapotea kisa tu kufanikisha demokrasia. Naomba nieleweke, tatizo hapa sio demokrasia bali tija ya chaguzi zetu hasa upande wa rais hususan Tanzania Bara.

  Tujiulize ni fedha kiasi gani zinatumika kuanzia uandikishaji ktk daftari la wapigakura, mchakato wa mzima wa kampeni na mpaka siku ya kupiga kura...ni fedha nyingi sana ambazo zingeweza kutatua matatizo mengi sana ya hii nchi. Naomba nieleweke tena sina tatizo ktk chaguzi za madiwani na wabunge ila tatizo langu lipo ktk uchaguzi wa rais. Kwa mfano ni obvious kuwa hata wapinzani wenyewe wanafahamu kuwa Kikwete atashinda ktk uchaguzi huu, na Kikwete anashiriki ktk uchaguzi huu ili kuvunja rekodi yake ya ushindi wa 80% ya mwaka 2005 ila na yeye anafahamu kuwa lazima ashinde but still tunahangaika as if hatufahamu jambo hili.

  Ushauri wangu ni kuwa kwa nafasi ya rais uchaguzi uwe unafanyika kila baada ya miaka 10 mpaka hapo watanzania tutakapofikia level ya demokrasia ya wenzetu waliofikia hatua ambayo hadi siku ya upigaji kura mshindi bado anakuwa hajafahamika.
   
 2. Kikojozi

  Kikojozi JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2010
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 331
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu,

  Baada ya kushuhudia matukio ya wiki chache zilizopita kama vile Mrema wa TLP kuhudhuria mkutano wa CCM an CHADEMA kupokea kwa mikono miwili msaada wa fedha kutoka kwa mfanyabiashara Sabodo ambaye ni mwanachama "damu" wa CCM, nimegundua kwamba vyama vyetu vya siasa ni usanii mtupu.

  Pia hizi chaguzi zetu ambazo chama tawala kinatangaza uhakika wa kushinda miaka kabla ya uchaguzi wenyewe na kila mtu kuitikia wito naona ni jambo la mzaha.

  Mimi napendekeza katiba ibadilishwe kufuta chaguzi na vyama vya siasa vyote hapa nchini. Badala yake tuwe na utawala wa kifalme na mfalme au malikia atakayetawala maisha na atakua anateua wasaidizi wake kutawala majimbo.

  Tukifanya hivi kwanza tutaokoa matrilioni ya fedha zinazopotea katika kugharimia chaguzi na kuvilipa vyama vya siasa ruzuku. Hizi badala yake zitawekezwa kwenye sekta muhimu kama elimu, afya, nishati na miundombinu.

  Pili, uchumi utakua kwa kasi ya ajabu kwasababu wale watu wote waliokua wanajihusisha na malumbano yasiyokua na tija chini ya kivuli cha siasa sasa wataelekeza nguvu na maarifa yao kwenye shughuli nyingine za ujenzi wa taifa kama vile uhandisi, utabibu, ualimu, biashara na michezo.

  Ikiwa huu utawala wa kifalme utashindwa kusimamia maendeleo yetu na kukidhi mahitaji yetu kiasi cha kuamsha hasira na hisia kali ndani yetu sisi wananchi wa kawaida, basi tutaupindua na hapo ndipo DEMOKRASIA YA KWELI itakapozaliwa.

  N
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kwa kuanzia tumtawaze Kikwete kuwa mfalme kisha akifa Ridhiwan achukue nafasi yake.
   
Loading...