Uchaguzi Simba waahirishwa na TFF......

Uchaguzi Simba waahirishwa na TFF......

Blood Hurricane

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2012
Posts
1,175
Reaction score
305
Kwa mujibu wa TFF INATAKIWA kuundwa kwa kamati ya Maadili ambayo mpaka sasa haina wajumbe kwa mujibu wa katiba mpya ya Simba s.c iliyopitishwa hivi majuzi.
Tarehe ya uchaguzi itapangwa upya.
Sarakasi zingine hizi......
Nawasilisha.

===============
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kusimamisha uchaguzi wa Simba uliopangwa kufanyika Juni 29.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi amewaambia waandishi wa habari hivi punde kwamba wamesimamisha uchaguzi huo na kuiagiza Simba kuunda kamati ya maadili.

Baada ya hapo, rufaa zilizokatwa na wanachama wakiwapinga baadhi ya wagombea zitapelekwa kwenye Makati hiyo.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari leo kwenye makao makuu ya TFF katikati ya jijini la Dar es Salaam, Malinzi alisema TFF wameona huenda utaratibu unavyokwenda unaweza kuathiri uchaguzi huo.

"Hivyo TFF inawaagiza Simba kuunda kamati ya maadili ambayo itachukua uamuzi wa kuyashughulikia malalamiko ya wanachama baada ya mchakato wa kamati ya uchaguzi.
"Lakini ikitokea kuna watu hawajaridhishwa na hilo, basi moja kwa moja watakata rufaa kwenye kamati ya maadili ya TFF," alisema huku akitaja kutumia katiba ya Simba ibara ya 16 kifungu 1(e) na ibara ya 30 kifungu (h).

Baada ya kamati ya uchaguzi ya Simba kukamilisha michakato yote, rufaa ziliwasilishwa kwenye kamati ya rufaa ya TFF ambayo ilitoa uamuzi wa kumrudisha mgombea wa Urais Michael Wambura.

Lakini wanachama wengine wakakata rufaa wakianisha mambo kadhaa likiwemo suala la Wambura kugushi barua ya katibu mkuu wa zamani wa Simba, Evodius Mtawala kama ambavyo Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Simba, Dokta Damas Daniel Ndumbaro alivyosema.

Kutokana na hali hiyo, suala limeonekana kuwa gumu na TFF inalirudisha suala hilo Simba kwa maana moja au nyingine.

Wacha waendelee kuwa chini ya Al shabaab a.k.a mzee wa pistol
 
wanasoka tuhamieni kwenye muziki tu.
 
Kwa mujibu wa TFF INATAKIWA kuundwa kwa kamati ya Maadili ambayo mpaka sasa haina wajumbe kwa mujibu wa katiba mpya ya Simba s.c iliyopitishwa hivi majuzi.
Tarehe ya uchaguzi itapangwa upya.
Sarakasi zingine hizi......
Nawasilisha.

Bora hayo matimu ya simba na yanga yaanze kufa taratibu ndo yanaharibu soka letu
 
Kwa mujibu wa TFF INATAKIWA kuundwa kwa kamati ya Maadili ambayo mpaka sasa haina wajumbe kwa mujibu wa katiba mpya ya Simba s.c iliyopitishwa hivi majuzi.
Tarehe ya uchaguzi itapangwa upya.
Sarakasi zingine hizi......
Nawasilisha.

Baadae watakumbuka hata kamati ya rufaa haipo walitumia ya TFF?
 
Kwa mujibu wa TFF INATAKIWA kuundwa kwa kamati ya Maadili ambayo mpaka sasa haina wajumbe kwa mujibu wa katiba mpya ya Simba s.c iliyopitishwa hivi majuzi.
Tarehe ya uchaguzi itapangwa upya.
Sarakasi zingine hizi......
Nawasilisha.

Piga ua Matajiri wanaojiita friends of simba hawatakubali Wambura agombee uchaguzi SSC. Watatumia kila aina ya mbinu aenguliwa kugombea. Wanahisi akishinda utakuwa mwisho wao kuinyonya SSC katika kisingizio cha ufadhili. Haiingii akilini kuwa uamuzi wa kamati ya rufaa unapingwa kwenye chombo cha chini. Kwa sababu ikiwa ni kamati ya maadili, iwe ni ya SSC au ya TFF bado kimamlaka itakuwa sio juu ya kamati ya rufaa ya TFF.
 
You are right.
 
kwa mujibu wa tff inatakiwa kuundwa kwa kamati ya maadili ambayo mpaka sasa haina wajumbe kwa mujibu wa katiba mpya ya simba s.c iliyopitishwa hivi majuzi.
Tarehe ya uchaguzi itapangwa upya.
Sarakasi zingine hizi......
Nawasilisha.

watakoma unafiki na fitina za soka na uongozi dhidi ya wenyewe kwa wenyewe."siye yanga wa nyakato mwanza roho kwaatu!adui yako mwombee njaa.(hata mama mwanaidi wa kijiwe cha kahawa national aliwaasa kufanya uchaguzi bila mgawanyiko wa kimakundi).
 
Piga ua Matajiri wanaojiita friends of simba hawatakubali Wambura agombee uchaguzi SSC. Watatumia kila aina ya mbinu aenguliwa kugombea. Wanahisi akishinda utakuwa mwisho wao kuinyonya SSC katika kisingizio cha ufadhili. Haiingii akilini kuwa uamuzi wa kamati ya rufaa unapingwa kwenye chombo cha chini. Kwa sababu ikiwa ni kamati ya maadili, iwe ni ya SSC au ya TFF bado kimamlaka itakuwa sio juu ya kamati ya rufaa ya TFF.

Wanainyonya kivip? fafanua mkuu. Hata akigombea, hatuwezi mpa team WAMBURA hana tofauti na Ismail. Aliyewaambia FoS ni wezi, maadui ni nani?. Hatuewzi mpa team mtu ambae anashabikiwa na wapinzani wetu
 
kwani yule dr ndumbalu hakuliona hilo mpaka atangaze tarehe ya uchaguzi elimu yake magumashi nini?
 
Back
Top Bottom