Uchaguzi October 2010 Hautakuwa Huru!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi October 2010 Hautakuwa Huru!!!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by RedDevil, Aug 7, 2010.

 1. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  WanaJF, kama tulivyozoea kuoa chama tawala kikitumia pesa nyingi kuhahakisha kinashinda chaguzi mbali mbali hapa nchini. Ninaomba sasa tukubali kabisa kuwa uchaguzi mwaka huu hautakuwa huru na wahaki.

  Hili halina ubishi wala mjadala kwani tayari tumeona dalili kwa kuanza kura za maoni ndani ya chama tawala, yaani CCM. Kwa kuzingatia hili ninayo maombi yafuatayo!

  1) Ninaomba NEC itoe tamko rasmi kuwa mwaka huu uchaguzi hautakuwa huru na wa haki hivyo ni bora mwananchi ajipange kuhakikisha analinda kura yake.

  2)Wananchi wote wajulikane watakopiga kura kila sehemu na majina yao tuyahakiki haraka iwezekanavyo vinginevyo tutaendelea kupiga kelele "ufisadi" wakati tunaupenda sisi wewe wananchi.
  3) Kwa kura wananchi wengi watapiga kura mwaka huu,"assumptions" inabidi basi wananchi waruhusiwe kukaa kituoni hadi pale matokeo yatakapotangazwa.

  Ruksa kuongeza au kubadili kilichoandikwa.
   
 2. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2010
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ni hatua nzuri sana hiyo
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ndugu mtoa mada jambo la muhimu ni kuwahamasisha wananchi wawe tayari kupambana katika kuilinda kura ,kwa maana sio Slaa wala Lipumba ataweza kulifanya hilo ,hilo ni jukumu la kila mpiga kura kuwa matokeo ya kura yanakuwa ni ya halali na kama kura zilivyopigwa ndivyo zinavyotangazwa.
  Pemba walifanikiwa kuing'oa CCM kwa kuwa walikubali kuwa jukumu la kulinda kura sio la Chama wala mugombea ni jukumu la kila mwananchi au kila mwananchama ,na mchakato huu unaanza wakati wa uandikishaji na pia wakati wa kuhakiki daftari au majina ya wapiga kura wa sehemu husika idadi iwe inajulikana kabla ya siku ya upigaji kura,pia mawakala wa vyama ambao wapo ndani ya kituo cha upigaji kura hawa hawatakiwi kutokatoka au kuondoka kwa pamoja na ikiwa chama kina wakala shupavu basi akianzisha vurumai humo ndani ya chumba mlioko nje mtasikia kuwa ndani mambo si shwari ,wakala asienunulika ,hawa kule Pemba walifanikiwa na hawakwenda hata kukojoa ,walishinda humo na kukagua kila kitu kadiri ya sheria inavyomruhusu na walihakikisha wanapata majina yote au takwimu zote za wapiga kura katika kituo na mwisho walihakikisha kura zinahesabiwa kiuhakika kabisa ,kila aliechaguliwa basi kura yake anawekewa na mwisho zinahesabiwa na kisha kulinganishwa idadi ya kura zote zilizohesabiwa na idadi ya waliopiga kura katika kituo hicho. Ila huko Tanganyika mawakala wengi wananunulika na siku ya siku wengine hawaonekani ,utasikia wamepotea katika mazingira ya kutatanisha au hawakufika.Hapo ujue keshakatiwa chake na anatakiwa asihudhurie ajifiche kabisa asionekane kwa masiku.
   
Loading...