Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,103
- 128,718
Wanabodi,
Nimenote baada ya matokeo ya Kinondoni na Siha, kuna watu wanajifanya na kujidai wamekasirika sana!, na wako tayari kwa lolote na kufanya lolote kuiondoa CCM madarakani!. Ushauri wangu kwa watu wa type hii, ni kuwaasa kwa sasa wasijisumbue bure!, CCM is there to stay for a long long time!, kwasababu mpala sasa Tanzania hapa tulipo, bado hatuna any serious opposition, ya kuiondoa CCM madarakani, labda mpaka 2030, ndipo CCM itaanza tena kutikiswa tikiswa na opposition ili kufungashwa virago, viginevyo CCM itaendelea kutawala na probably, itatawala milele nchini Tanzania if nothing changes!.
Siasa ni sayansi, kuna sayansi ya siasa. Kinachoifanya CCM iendelee kushinda chaguzi mbalimbali na kuendelea kutawala ni matumizi sahihi ya mtaji mkuu wa CCM ilionao, ambao ni watu, na haswa wa vijijini, ambako CCM ime invest a lot on ignorance na lindi la umasikini wa kutupa uliotopea, hivyo as long as mtaji huu upo, na unaendelea kuwepo, CCM itaendelea kutawala daima dumu!.
Kufuatia idadi kubwa ya Watanzania walio wengi, wanaishi vijijini kwenye lindi la umasikini uliotopea na ambao wengi wao ni watu goi goi wajinga wa kutupa, walioishia darasa la saba, hivyo hawajui huwa wanachagua nini!, hawa wataendelea kuichagua CCM mwaka hadi mwaka na kila uchao!.
Idadi ya goi goi na wajinga hawa ni kubwa kuliko idadi ya Watanzania werevu, wanaojitambua na kuwa na uwezo wa kufanya kitu kinachoitwa "informed decisions", hivyo watu wanaichagua CCM kwa mazoea tuu, na kuna maeneo CCM hata ikisimamisha jiwe, jiwe litapita.
Kufuatia rais Dr. John Pombe, Joseph Magufuli kutoa elimu ya bure kwa Watanzania wote, batch ya kwanza ya wanafunzi walioanza darasa la kwanza la bure, watapiga kura kwa mara ya kwanza uchaguzi wa mwaka 2030, hivyo hawa hawatakuwa wajinga wajinga tena!
, wa kupelekwa pelekwa kama mazuzu!, na Tanzania ya viwanda, mapinduzi ya kilimo na uchumi wa gesi, utaigeuza Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati, hivyo kupunguza ule umasikini uliotopea, sasa huu ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa CCM!.
Angalizo: Nimesema ni mwanzo wa mwisho wa CCM, sijasema ni mwisho wa CCM!. Hivyo kipindi chote hiki kutoka sasa hadi hiyo 2030, CCM haitajikalia tuu hivi hivi tuu kusubiria kufa kibudu, CCM wakati wote itakuwa busy kutekeleza ilani yake ili muda wa uchaguzi ulifika, CCM iibuke na kusema tuliahidi, tumetekeleza, hivyo kuzidi kujiimarisha ili kuendelea kutawala milele!.
Wengi wa wajinga wajinga waliokuwa wanaichagua CCM kwa mazoea tuu, most of them will have been long gone! na masikini wa kutupwa wenye kuweza kuuza kura yao kwa T-shirt na kofia, na shibe ya siku moja, watakuwa wamepungua!, mimi mwenyewe will be at 60s!.
Hata hivyo sio wote wanaiochagua CCM ni wajinga wajinga, kuna wengine wenye akili zao timamu, wanaichagua CCM kwa sababu hakuna alternative, hatuna any serious, credible opposition to choose from, upinzani uliopo ni upinzani uchwala. Wapinzani hawana hoja, wanatumia hoja za nguvu, badala ya nguvu za hoja, wamekalia siasa za matukio!.
Wapinzani mtanisamehe kuwaita Upinzani Uchwala, kwa sababu huu ndio ukweli wenyewe!. CCM ilikwisha chokwa siku nyingi ila kukosekana kwa upinzani imara kumewakatisha tamaa waliowengi na kuamua kutokupiga kura, badala ya kupoteza muda!, kwa sababu haoni cha kuchagua!.
Upinzani uliopo ni upinzani wa kupinga kila kitu, kupayuka, kutukana na kuhamasisha chuki, na uvunjifu wa amani kwa kutumia hoja za nguvu, badala ya kutumia nguvu za hoja, Upinzani wa kweli ni upinzani wenye hoja mbadala. Upinzani huu tulionao, bado haujaonyesha ukomavu wa kutosha kuaminiwa na kukabidhiwa ikulu yetu, hivyo japo CCM ni Li Zimwi, hili ndilo zimwi Watanzania walijualo!.
Hivyo wale wote wenye hasira na CCM, nawashauri washushe pressure zao, kwa sasa kwa siasa za Tanzania, mpango mzima ni CCM, uchaguzi wa 2020, karibu majimbo yote yaliyokuwa yanashikiliwa na upinzani, yatarejeshwa CCM, na Tanzania kuwa nchi ya chama kimoja, kwa miaka 10, kuanzia 2020 hadi 2030.
Hiki ni kipindi cha upinzani kujijenga upya, kwa kuhakikisha, tunabadili sheria ya uchaguzi, kuutoa ujinga wa kudhaminiwa na vyama na kuruhusu wagombea binafsi, tunasawazisha uwanja wa mchezo wa siasa kwa kutengeneza a level playing field, ili kufanya uchaguzi katika ushindani sawia, na kuifanyia maboresho Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo japo ni Tume Huru ila sio Inclusive, hivyo Tume itafanywa more inclusve ili kuwapata viongozi wasio na vyama, na makamishna, wajumuishe wawakilishi wa vyama vikubwa angalau toka vyama vitatu vikuu. Na hapa sasa ndio tutaona kuibuka kwa upinzani wa kweli ambao utaanza tena 2030!.
I pray to God, to grant me the privilege to witness this day.
Paskali