Uchaguzi Mkuu wa Bavicha-Mwanahalisi laeleza kila kitu nyuma ya pazia

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Nimelisoma gazeti la leo la mwanahalisi.Nimekuwa nikifurahishwa na uandishi wa gazeti hili kutokana na umahiri wa waandishi wake.Pamoja na mambo yote mazuri yaliyoandikwa leo,nimefurahishwa na habari inayohusu uchaguzi mkuu wa Bavicha uliomalizika.Hakika kila kitu kimewekwa hadharani.Kuna mgombea mmoja ambaye alituhumiwa kutoa rushwa kwa wajumbe kupitia M-pesa na Tigo Pesa.Wengine tulidhani labda ni majungu tu yaliyosababishwa na wapinzani wake.Kumbe hisia zetu hazikuwa sahihi.Mwandishi wa gazeti la mwanahalisi Alfred Lucas ametoboa kila kitu,ameenda mbali kwa kutaja na kuziandika namba zote zilizopokea pesa hizo mpaka muda zilipotumwa.Hakika hii nimeipenda.Huu ndio uandishi na uchunguzi wa habari tunaoutaka.Hakuna atakayesimama na kusema niliondolewa kwenye mchakato kwa uonevu.Mambo yote yako hadharani.Hata wale Matomaso waliopenyeza uongo wa porini wataamini sasa...........
Hongera Mwanahalisi,waandishi wengine igeni mfano huu.
 
Siku zote mwanahalisi ni gazeti bora TZ mengine yanafuata.Wandishi wake hawa bahatishi.Tunaomba mwanahalisi muende Tarime-nyamongo mkatuletee ukweli
 
Habari Leo,mpoooo??? Jamba Leo,mpoooo???? Mkuchika upooooo???? Nnur,mpooooo???? UVCCM,mpooooo????
 
Ngoja nikakamate nakala yangu muda si mrefu, nadhan kuna mambo mazuri! Mwanzo Mwisho huwa naliwaza hilo gazatte!
 
Nalikubali sana mwanahalisi,hawabahatishi na wala hawaandiki habari za majungu,hawaandiki habari ili kuuza gazeti they rely on the truth...magazeti mengine igeni mfano huu...no one will come na kusema uchaguzi bavicha ulikuwa ni majungu isipokuwa magamba ambao wanafanya kila hila kuichafua chadema...big up mwanahalisi
 
wandugu wapenzi, wengine wenu tuko mbali kuweza kupata nakala ya hilo gazeti tunalolipenda. Ombi; mtumegee basi walau sehemu ya habari yenyewe ili tuwepamoja. NB: wanachelewa sana kuweka nakala yao kwenye ukurasa wao wa mtandao.
 
I miss this newspaper a lot jamani wahusika tunaomba muwe mnaliweka mtandaoni mapema tupo ughaibuni tunalikosa sana maana ndo gazeti linalozungumza upande mwingine wa watu
 
niwekeeni nakala hapa...ili nijue maana kuna yule kijana wetu humu jf juzi kajitetea sana........ole wake nikute jina lake mle kama alituma hizo tgo pesa na m-pesa......
 
wandugu wapenzi, wengine wenu tuko mbali kuweza kupata nakala ya hilo gazeti tunalolipenda. Ombi; mtumegee basi walau sehemu ya habari yenyewe ili tuwepamoja. NB: wanachelewa sana kuweka nakala yao kwenye ukurasa wao wa mtandao.

Nashauri mwenye nalo a-scan na kulitupia hapa jamvini.
 
mwanahalisi
Gazeti 1 la mwanahalisi=2888888xhabari leo

huwezi fananisha hilo gazeti na na hayamengine yanayofuata upepo hususani habari leo na kak yeke

mwanahalisi daima
 
Binafsi naikubali ya kazi ya kubenea na habari nimeisoma yote ni ukweli mtupu. Pia ni mwendelezo wa misimamo isioyumba ya Chadema kusimamia haki.
 
Nimelisoma gazeti la leo la mwanahalisi.Nimekuwa nikifurahishwa na uandishi wa gazeti hili kutokana na umahiri wa waandishi wake.Pamoja na mambo yote mazuri yaliyoandikwa leo,nimefurahishwa na habari inayohusu uchaguzi mkuu wa Bavicha uliomalizika.Hakika kila kitu kimewekwa hadharani.Kuna mgombea mmoja ambaye alituhumiwa kutoa rushwa kwa wajumbe kupitia M-pesa na Tigo Pesa.Wengine tulidhani labda ni majungu tu yaliyosababishwa na wapinzani wake.Kumbe hisia zetu hazikuwa sahihi.Mwandishi wa gazeti la mwanahalisi Alfred Lucas ametoboa kila kitu,ameenda mbali kwa kutaja na kuziandika namba zote zilizopokea pesa hizo mpaka muda zilipotumwa.Hakika hii nimeipenda.Huu ndio uandishi na uchunguzi wa habari tunaoutaka.Hakuna atakayesimama na kusema niliondolewa kwenye mchakato kwa uonevu.Mambo yote yako hadharani.Hata wale Matomaso waliopenyeza uongo wa porini wataamini sasa...........
Hongera Mwanahalisi,waandishi wengine igeni mfano huu.

Hili si ndilo gazeti la mwandishi wake Kubenea kununuliwa na RA ? hili limeisha kosa imani kwa watz
 
Back
Top Bottom