Mkuu, ukisikia mtu anaitwa "Bulldozer" basi huyo ni kama mitambo ya ujenzi wa barabara. Mtambo wa aina hii unafaa sana wakati wa ujenzi wa barabara, lkn barabara ikisha kamlilika, mtambo huu hautakiwi tena kutembea wenyewe barabarani, bali hubebwa na malori makubwa na tena tahadhari hutolewa iwapo unasafirishwa.
Nafikiri tunaona mtambo umeaminiwa kutembea wenyewe barabani. Unapondaponda kila kilichopo mbele yake. Si injinia wala dereva ambaye anaweza kuhoji kuhusu uharibifu ambao mtambo unaufanya.