Uchaguzi Mkuu 2020 bado miaka 2.5. Kila mtu atavuna alichopanda

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Wakuu.

Kabla hata sijasahau mvutano mkubwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, nimefikiria sana nikagundua uchaguzi ujao umekaribia sana, bado miaka 2.5 kipenga kipulizwe. Kisiasa ,muda huu ni mfupi sana kujipanga, unahitaji resources nyingi sana kukamilisha mchakato mzima.

Kwa nafasi ya Urais, kupanga safu nzima kuanzia ngazi ya Taifa mpk shina ni mchakato ambao ulitakiwa uwe unaendelea immediately baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Nchi ya Tanzania n kubwa sana, ina wasomi na wasiojua kusoma wengi sana.

Waliofanya vzr watavuna walichopanda. Na wale wenzangu wapiga dili, kukimbilia mijini kukimbia wananchi vijijini, wataipata. Kuna watakaotumia matukio mbalimbali kujisafisha kisiasa.

Km umewatumikia wananchi, utatoboa. Km ulijifanya mjuaji, tunakunyima kura. Hata ukiiba hazijai.

Kila la kheri.
 
Lakini tume ya uchaguzi ndio wataamua rais wetu kwa kumtangaza mshindi. Ndio maana watu haiwasumbui sana uwajibikaji.
 
Hahaaa.....mbona hatupati update ya mradi wa reli?

Nasikia hakuna hata greda moja linalofanya kazi saiti,ilikuwa kiki ya harmorappa?
Mkuu nahisi hata mkandarasi hajapatikana..
Waliweka jiwe la msingi in advance..
Ndio madhara ya kuzungukwa na washauri type ya Bashite.
 
Mengeleni mi najua huwa unapoint sana,leo umekula nini hadi unajipotezea heshina hivi.
kweli siamini kama hujui katika ujenzi mkubwa kama huu vifaa vingi vya kufanyia kazi either vinahamishwa toka mbali au kununua,hivyo lazima kuwepo na mobilization period,
Hapo site utaona iko kimya lakini kuna kazi kubwa sana inafanyika.mfano kusafirisha vifaa,kununua vifaa vipya,
kuorganize staff,kuricrute wafanya kazi, kukodi wstaalam.kuweka mahusiano mazuri na mabenki.etc.usibeze ukiona kimya ,hiyo sio sa na kujenga barabara zetu za vumbi.
vifaa viko majini vinakuja,!"!
 
Vyama vya upinzani ni vyama vya msimu (seasons parties)
wakati wa uchaguzi mkuu tu
Tunategemea season kuanza the end of 2019.
 
Back
Top Bottom