Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema Uchaguzi Mdogo katika Majimbo ya Konde (Mkoa wa Kaskazini Pemba) na Ushetu (Shinyanga) utafanyika Oktoba 09, 2021
Wagombea watachukua fomu kuanzia 13-19 Septemba, uteuzi utafanyika Septemba 19 na Kampeni zitaanza 20 Septemba hadi 08 Oktoba
Jimbo la Konde lipo wazi baada ya Mbunge Mteule kujiuzulu na aliyekuwa Mbunge wa Ushetu na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa , Elias John Kwandikwa alifariki dunia Agosti 02
Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo ineyangaza mchakato wa Uchaguzi katika Majimbo ya Ushetu mkoani Shinyanga na Konde Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo Uchaguzi huo umepangwa kufanyika Oktoba 9,2021.