GE2025 Uchaguzi mdogo Fuoni na Siha kufanyika leo

GE2025 Uchaguzi mdogo Fuoni na Siha kufanyika leo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele, leo Desemba 29, 2025 ametoa taarifa kuhusu uchaguzi mdogo wa ubunge unaotarajiwa kufanyika Desemba 30, 2025 katika Jimbo la Siha, Mkoa wa Kilimanjaro (Tanzania Bara) na Jimbo la Fuoni, Mkoa wa Mjini Magharibi (Tanzania Zanzibar).

Amesema uchaguzi huo utahusisha pia kata tano za Tanzania Bara ambazo ni Chamwino (Manispaa ya Morogoro), Mbagala Kuu (Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam), Nyakasungwa (Wilaya ya Buchosa, Mwanza), Masoko (Wilaya ya Mbeya) na Ndono (Wilaya ya Uyui, Tabora).

Kwa mujibu wa Jaji Mwambegele, jumla ya wagombea 33 kutoka vyama vya siasa 17 wanawania nafasi za ubunge na udiwani, wakiwemo wanaume 21 sawa na asilimia 63.64 na wanawake 12 sawa na asilimia 36.36. Jumla ya wapiga kura 218,024 waliopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wanatarajiwa kushiriki uchaguzi huo, huku vituo 556 vya kupigia kura vitatumika.

Aidha, amevikumbusha vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi huo kuweka mawakala katika vituo vyote vya kupiga, kuhesabu na kujumlisha kura na kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo ya Tume wakati wa zoezi zima la uchaguzi.
1767074684724.png
 
Back
Top Bottom