HILLARY CLINTON AFIKIA MAGIC NUMBER 2383+
MAJIMBO 6 KATIKA UCHAGUZI LEO HII
Kama alivyosema Mkuu
Mag3 CNN nao wametangaza Clinton kafikia namba 2383+ 1
Habari hizi zimekuja katika usiku wa kuamkia uchaguzi wa majimbo 6 siku ya Jumanne
Wafuatiliaji wa mjadala wameuliza, imekuwaje namba imefikiwa kabla ya kura kwa majimbo ya Montana, North and South Dakota, New Mexico, New Jersey na California?
Kumbuka idadi ya 2383 ni wajumbe wa kuchaguliwa na wajumbe wa Super Delegates
Katika idadi ya mwanzo ya Super delegates kuna kiasi kilichobakia ambacho hakikuchukua upande. Idadi kamili ya SD wanaoingia katika mkutano mkuu ni 15%
Kwa siku mbili wengi wanajiuliza nini kimetokea. Well, baadhi ya SD wamemuunga mkono Hillary kama walivyomuunga Sanders na kufikia 47.
Hawa ndio wamesukuma gurudumu la Hillary kufikia hapo lilipo.
Habari za Clinton kufikia namba hiyo zilijulikana kama wiki moja kwa kufuatilia wajumbe
Hata hivyo zimetangazwa leo ikiwa ni katika 'namna ya Sanders na vyombo vya habari'
Kutangazwa habari hizi ni kuwafanya wapiga kura wa Clinton wabweteke na pengine kutojitokeza. Hilo litasaidia Sanders kushinda maeneo mengi na hasa California
Ushindi wa Sanders California utajenga hoja yake ya kukubalika katika majimbo makubwa. Kwa idadi ya viti vinavyomchagua Rais wa Marekani , California ina viti vingi(electoral college).
Hivyo Sanders atajenga hoja kuwa inaonekana wazi kukubalika
Hapo ataendelea na hoja yake ya kwenda Philadephia.
Ingawa pia habari hizi zinaweza kumrudi kwa kukatisha tamaa wafuasi wake, ukitazama kwa undani Sanders alijua hilo na kulifanyia maandalizi mapema
Mikutano mingi amejenga wafuasi wake wakubali kuwa njia ni ngumu ila kuna namna moja, kwamba wakishinda California ngoma itakwenda mkutano mkuu
Wafuasi wa Sanders watapigana kuhakikisha hilo linatokea, wa Clinton watabweteka
Kwa mantiki hii, tunaweza kubashiri ifuatavyo
California: Mshindi atakuwa Sanders
New Jersy: Mshindi atakuwa Hillary Clinton
Dakota (south and North) : Sanders
Montana: Sanders atashinda
New Mexico: Clinton atashinda
Kwa matokeo hayo, ni unlikely Sanders anaweza kutangaza kuvunja kampeni.
Ingawa amefikiwa na Obama kwa simu, hakuna ajuaye nini maongezi yao
Kwa Clinton, endorsement ndizo zitaweza kumnyamazisha Sanders.
Tutaendelea