Sijui wamechanganyikiwa nini - mdukuzi anawezaje kufanikiwa kuingilia mifumo ambayo haijafungwa kwenye mtandao i.e Internet - mama mwenye kasema mfumo wao ni imara sana hawezi kuingiliwa na Taifa lolote, lakini bado maadui wa Trump wanakuja na ngonjera eti majibo 21 yalijaribiwa kuingiliwa na Urusi lakini hawana ushahidi wowote wanatapa tapa tu kama watoto wadogo!!!
Taifa linalo heshimika linataka kujidhalilisha kwa madai ya kipuuzi maadui wa Trump wanajifanya kuwa paranoid na Urusi mara Urusi this Urusi that - lengo lao hawataki Trump hawe na mahusiano mema na Putin kwani hilo linaweza kufanya viwanda vya silaha vikose soko ndiyo maana muda wote Amerika upendelea sana kubuni adui ili wapate kisingizio cha kutaka kuingia kwenye ushindani wa kuhunda silaha na mataifa hasimu - uadui wao na baadhi ya Mataifa mengine utakuta mara zote ni wa kuchonga tu - the problem is they never saw it coming kwamba watashindwa uchanguzi.
Si wanajifanya ni wastaarabu na wana demokrasia, sasa kama Hillary alikubali matokeo tangu mwanzo bila ya kushinikizwa na MTU kwamba Trump alishinda kihalali, sasa mbona yeye na mumewe wakishirikiana na akina Obama wanakula njama ili TRUMP aondolewa madarakani kwa visingizio vya kutunga tu vinavyo chochewa na MSM za nchini mwao, wanakwenda mbali na kuchochea Mataifa ya Ulaya yamuone Trump hafai - hii ni ajabu kweli kweli!!
Hillary, mumewe, Obama na wengine wakae wakijua kwamba kilicho wapata kinatokana na Wapiga kura wa Marekani kuchoshwa na kundi hilo hivyo raia wakahamua kufanya mapinduzi ya kimya kimya kupitia sanduku la kupigia kura, wakamchagua mtu ambaye hayumo kwenye kundi la Establishment ambalo ujiona ndilo lenye hati miliki ya kuwatawala watu wengine miaka nenda rudi.