Uchaguzi CCM Sumaye apaniwa Hanang | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi CCM Sumaye apaniwa Hanang

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 18, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [h=2]17 JULY 2012 [/h]Na Reuben Kagaruki

  WAKATI mchakato wa chaguzi mbalimbali ukiendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuna taarifa kuwa katika Wilaya ya Hanang’, mkoani Manyara, hali si shwari.

  Mchuano mkali unararajiwa kuwepo katika kinyang'anyilo cha kumpata Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), kutoka wilayani humo.

  Habari za uhakika ambazo zimelifikia gazeti hili, zinasema joto la uchaguzi huo limepanda baada ya kuvuja taarifa kuwa, Waziri Mkuu mstaafu katika Serikali ya Awamu ya Tatu, Bw. Frederick Sumaye, ameamua kugombea nafasi ya NEC, ngazi wa Wilaya.

  Hivi karibuni, Bw. Sumaye alikaririwa akikosoa utendaji wa baadhi ya viongozi wa CCM, katika Sekreterieti iliyopita ambayo ilikuwa ikiongozwa na Katibu Mkuu, Bw. Yusuf Makamba.

  Bw. Sumaye aliwataka viongozi hao kutokaa kimya badala yake wajibu hoja mbalimbali zinazoelekezwa kwao na wapinzani ili kutovipa umaarufu vyama hivyo kwa umma.

  Kauli hiyo ya Bw. Sumaye ilikosolewa na baadhi ya viongozi walioguswa, wengine kumwona kama mpinzani na kumtaka ajiunge na vyama pinzani.

  Inadaiwa kuwa, Bw. Sumaye ameamua kwenda wilayani Hanang kugombea nafasi hiyo ili kujihakikishia ushindi.

  Marekebisho makubwa yaliyofanywa na CCM hivi karibuni ni pamoja na kupitisha utaratibu wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho kuchaguliwa katika ngazi ya Wilaya ili kukijenga zaidi chama kwa wananchi.

  Hata hivyo, vyanzo vyetu ndani ya CCM vimedai kuwa, wakati, Bw. Sumaye akijiandaa kwenda Hanang’ kugombea nafasi hiyo, tayari wapinzani wake kisiasa wamejipanga kumuunga mkono kogogo mmoja maarufu wilayani humo ili akapambane naye.

  “Baada ya wapinzani wa Bw. Sumaye kisiasa kubaini hatagombea kupitia nafasi za kapu na kuamua kwenda wilayani kwake, wamemshawishi (wanataja jina), ili akapambane naye,” kilisema chanzo chetu ndani ya CCM.

  Mbali na kukikosoa chama chake, Bw. Sumaye ambaye alikuwa miongoni mwa wana CCM 11 waliojitokeza kugombea urais kupitia chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, amekuwa akitajwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa ana mpango wa kugombea urais mwaka 2015 baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza muda wake wa kikatiba.

  Wachunguzi wa mambo ya siasa wanadai huenda mtazamo huo unachangia mahasimu wake kisiasa kuhakikisha wanamkwamisha mapema ili asifikie malengo hayo.   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Nilidhania Sumaye na Siasa basi; Sasa anarudi NEC na halafu nini tena?
   
 3. k

  king11 JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ​kwanini asingegombea ukatibu au unaibu katibu wa CCM wilaya ambao moja kwa moja wanaingia NEC?
   
 4. Baba Collin

  Baba Collin JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  magamba magumu hayo
   
 5. only83

  only83 JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180

  Raisi anayekuja anamfahamu JK peke yake na hawezi toka kaskazini-UVCCM Pwani.
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Jul 18, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Waacheni wafu wawazike wafu wao! wao wanajipanga kivyama na chadema wanajipanga kuchukua nchi!
  Oh my God! kuna tofauti kubwa sana
   
 7. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  HAPPY BIRTHDAY MANDELA!(Avatar yako)
   
 8. d

  dandabo JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 303
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  kama wameweza kumtaja Sumaye, kwanini na huyo kigogo asitajwe? Kulikoni waandishi wetu?
   
Loading...