Uchaguzi 1995, hata Mrema aliibiwa kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi 1995, hata Mrema aliibiwa kura

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by kilemi, Oct 13, 2010.

 1. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nimesikia mara kwa mara B.W Mkapa na Kinana wakijibu waandishi wa habari kuwa ushabiki wa Dr Slaa sio kitu, eti kwa sababu uchaguzi wa 1995 "hata Mrema alikuwa hivyohivyo".
  Sina ushabiki wowote kwa sasa ila nimekasirishwa kwa kauli hizo kwa sababu mimi ni mmojawapo ya walioshindwa kupiga kura baada ya kusubiri kituo cha kura kwa siku mbili bila kupiga kura kisa eti ni shahada ziliisha. Kwa wanaokumbuka vituo vya kupigia kura vya mijini vilikuwa na matatizo yanayofanana, mpaka leo hakuna anayefahamu ya shahada zilikopelekwa, na mji kama Dar kura zilirudiwa!
  Nilikuwa Dodoma wakati huo, mawakala wa vyama vya upinzani hawakulipwa hela zao hadi leo, na walipodai kwa nguvu waliwekwa ndani kwa siku mbili, baadae wakaachiwa huru baada ya mlalamikaji kutokuonekana.
  Kwa mazingira kama yale Mkapa na kinana watadhubutu kuufananisha uchaguzi ujao na ule wa 1995?
  Je watabana shahada za kura na kusingizia kuwa uchaguzi umekuwa kama enzi za Mrema?
   
Loading...