Kwa niaba ya Wananchi wanaoishi Nyakato National kando kando ya barabara iendayo Buswelu, tunaendelea kuathirika kwa kiasi kikubwa na uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na vumbi zito na kelele za magari yanayokwenda na kutoka Buswelu baada ya kuwa Makao Makuu ya Wilaya ya Ilemela kujengwa eneo la Buswelu na kupelekea wananchi wengi kujenga nyumba zao za makazi karibu na Makao Makuu ya Willaya.
Athari tunazozipata ni kama yafuatayo:-
Athari tunazozipata ni kama yafuatayo:-
- Kelele nyingi za magari kwa muda wote wa masaa 24 na kutufanya kukosa usingizi kabisa.
- Wananchi na hasa watoto wetu kuugua magonjwa mbalimbali kama kikohozi, mafua, tumbo na kupelekea kutumia gharama kubwa kwa ajili ya matibabu.
- Kushindwa kufanya biashara hasa wenye mahoteli na kupelekea wateja wetu kutuhama kutokana vumbi zito.
- Vifaa kama friji, mashine za kupoozea hewa kuharibika mara kwa mara kutokana na vumbi zito.
- Vyakula vinavyotayarishwa majumbani mwetu kujaa vumbi na kupelekea vyakula hivyo kutokuwa salama kwa matumizi ya binadamu.
- Mavazi, Mashuka yetu kuchafuka kila mara na kutupa gharama kubwa kuyaweka katika hali ya usafi.
- Kutumia gharama kubwa ya maji kwa ajili ya kupunguza vumbi katika maeneo yetu
- Kuchafuka kwa kuta na paa za nyumba zetu na kuingia gharama ya kila mara kwa ajili ya ukarabati.
- Hatari kwa watoto wetu kugongwa na magari wanaosoma kwenye shule za msingi zilizoko kando kando ya barabara hiyo