Uchafuzi wa mazingira tarime | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchafuzi wa mazingira tarime

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Muke Ya Muzungu, Mar 23, 2010.

 1. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  john mashaka aibuka, safari hii kwa kimatumbi...


  Ndugu zangu watanzania, kila binadamua ameumbwa na haki sawa. Tumeumbwa kupendana na kuishi kwa furaha na amani. Haijalishi masikini au tajiri, haki za msingi za kibinadamu hazitambui nafasi ya mtu katika jamii. Wote tuna haki sawa ya kuishi maisha yenye afya furaha na amani.

  Kwa minajili hiyo hatuwezi kuukana na kuchelea ukweli kwa faida ya kitambo, Uwoga na tama vimefunika macho yetu wanajamii kwa ujumla pamoja na viongozi wetu kiasi kwamba mazingira yetu yanaharibiwa, na hata wanajamii wenzetu wanakufa pasipo sauti za kulaani vitendo hivyo viovu

  Katika muda wa wiki moja na nusu, nimepokea jumla ya emails 39 kutoka kwa watanzania mbali mbali wakinisihi kutafuta mbinu ya kuwasaidia ndugu zetu wilayani Tarime ambao wanahathirika na magonjwa ya ajabu ambayo yanatokana na uchafuzi wa Mazingira.

  Kusema kweli, picha zinazotoka huko, zinatisha na binadamu yeyote mwenye akili timamu au hutu kamwe hawezi kunyamaza. Kama wengi wenu mnavyofahamu, binafsi sina nguvu wala madaraka ya aina yoyote katika nchi yetu, ila kutokana na sauti za wengi, nimeamua kuwaandikieni ili tujadili kwa pamoja namna au jinsi tunavyoweza kushirikiana kama watanzania ili kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa matatizo yetu

  Hatuwezi tena kuwategemea wanasiasa wetu, kwani wametusaliti. Baadhi ya wanaharakati waliokuwa mstari wa mbele kutetea wanyonge, wamegeuka kuwa makada wa mashirika ya kigeni yanayochafua mazingira yetu. Yupo mmoja ambaye majuzi tu aliweza kutamka wazi kwamba Taasisi za kitanzania ziweze kununua hisa za makampuni Fulani huko Uingereza huku wananchi na wamiliki wa mali zinazofanyiwa biashara huko Uingereza wanakufa. Hatuwezi tena kuwaamini viongozi kama hawa; muda umefika kwetu sisi kutafakari hatima yetu wenyewe

  Nawaombeni wenye ushahidi wa aina yoyote kutuma ili tuweze kuvifikisha kwenye vyombo husika nchini Canada (Canadian Senate) na pia katika taasisi ya dunia ya haki za binadamu. Lazima tuwe tayari kujitoa mhanga katika kukupigania haki zetu za msingi. Yaliyotokea Balluchistan, Chile na New Guinea yanatokea Tanzania. Ikibidi sheria za kimataifa kuhusu " mauaji ya alahiki" zitumike kuvileta makampuni yanayo waua wananchi wetu mbele ya sheria.

  Maisha yetu siyo ramisi. Ingawa wengi wetu ni masikini, lakini haki zetu za kibinadamu ni vitu ambavyo lazima tuwe tayari kuvipigania kwa nguvu zetu zote na kwa njia zote zile chini ya uongozi wa kisheria.

  Tanzania, ndio moja ya taifa pekee duniani ambayo wananchi wake wanauwawa, na viongozi wake (wasaliti) wakabaki kimya. Lazima tuondokane na adui yetu uoga ili tuweze kushinda unyanyasaji unaofanywa na mashirika haya yanayotuchafulia mazingira na kuhatarisha maisha yetu. Hatuwezi kuwa waoga na kisha tukajiita binadamu na wazalendo.


  Kwani binadamu ambaye hayupo tayari kufa kw akutetea haki yake, hana maana ya kuishi. Hawa waathirika hawana hatia, dhambiyao kubwa ni kuzaliwa masikini kwenye jimbo lenye madini mengi. Ikiwa serikali yetu haitatusikiliza, basi Stephen Harper, itabidi atusikilize ila hatuwezi kunyamaza tena, dunia lazima isikie ukatili wanaofanyiwa ndugu zetu wa Tarime na kwingineko

  Mtanzania Mungu Ibariki Tanzania
  John Mashaka
  mashaka.john@yahoo.com


   
 2. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  john mashaka aibuka, safari hii kwa kimatumbi...  Ndugu zangu watanzania, kila binadamua ameumbwa na haki sawa. Tumeumbwa kupendana na kuishi kwa furaha na amani. Haijalishi masikini au tajiri, haki za msingi za kibinadamu hazitambui nafasi ya mtu katika jamii. Wote tuna haki sawa ya kuishi maisha yenye afya furaha na amani.
   
Loading...