Wana JF nawaomba ushauri wenu kuhusiana na jiji la Arusha kuwa chafu kupindukia! hakuna magari ya kubeba uchafu hivyo uchafu umetapakaa kila mahali. kumekuwa na vikao vya wananchi na madiwani wao kuzungumzia suala hilo lakini wale wenye magari wanadai kuwa wananchi hawalipi ada kwa ajili ya huduma hiyo lakini si kweli kwamba wote hawalipi kuna wanaolipa na wasiolipa. Nimekuwa najiuliza utaratibu gani utumike ili kuondokana na kadhia hii. Hali inatisha jamani kila pembe kuna lundo la takataka! Naamini michango yenu itafika kwa wahusika kwani wengi huwa wanachungulia humu.
Wana JF mnaoishi Arusha mtaniunga mkono kwa hili kwani hali halisi mnaijua.
Usiwape sababu ya kutafuna pesa za walipa kodi, dawa ya mtu mchavu ni kumlazimisha kuwa msafi siyo kumtembeza akaone show za wasafi.Arusha ni pachafu kweli. Kuna ulazima wa meya kwa kushirikiana na mkurugenzi wa jiji watembelee Manispaa ya Moshi then waje wakafanye kuiga. Jiji chafu sana hasa sewarge system, mtaani vinyesi kedekede kama vya biashara.
Tulitunze jiji letu.
Ulitegemea kitu tofauti kutoka kwa wamasai, na 'chotara' zao wameru na waarusha?geneva ya afrika chafu,kazi kwelikweli
Mbunge anayezoa taka majumbani? Nafikiri kuna haja ya serikali kurudisha kisoma cha elimu ya watu wazima na kuwalazimisha watu wote kusoma, hasa hasa somo la uraia.Muulize mwakilishi wetu mbunge siku akitoka kumsakama zitto dar
nilijua ni uchafu wa ngono. kumbe takataka. hata kwetu zipo