Kaka
JF-Expert Member
- Nov 22, 2006
- 742
- 371
Wadau,
Muda huu hapa maeneo ya Ubungo Darajani (Riverside) kuna matairi yamechomwa barabarani, askari wanafyatua risasi hewani. Kwa ufupi ni tahayari na taharuki.
Mwenye kujua atuarifu
Muda huu hapa maeneo ya Ubungo Darajani (Riverside) kuna matairi yamechomwa barabarani, askari wanafyatua risasi hewani. Kwa ufupi ni tahayari na taharuki.
Mwenye kujua atuarifu
Mi najua sema ngoja kwanzaa, niko hapa
Ishu ni kwamba jana mama lishe walipigwa sanaaa, machinga wakafukuzwa na kuna uvumi ni UKAWA na meya wa jiji hili. Sasa hapa walikuja mchana, wakajadili vizuri tu kuwa waache mama lishe wauze leo sababu washapika kesho kwa hiari hawatopika wala kuja. Mi nilikuwepo na ndugu yangu hapo kaniletea HG ndo nikawa namchukua sasa.
Wakakubali wakawa wanaondoka wanaenda SONGAS. Weeeeeeeee! Wahuni wakaanza kuwapopoa mawe wale sijui mgambo sijui FFU kwenye canter wakarudi sasa, tumekula mabomuuuuuu ya machoziii. Tumekula barutiiii, Maji ya kuwasha. Ndugu yangu anafoucs kwenye chakula kuokoa kanirushia mwanae. Tukawa tumetawanyana msichana wa kazi wala huyo ndugu yangu sijui walipo mpaka mda huu, simu haipatikani.
Kukawa shwari tu kwa dakika kadhaa, nikarudi kumrudishia mtoto wake maana nikajua tumbo limembana huko hajui mwanae alipo. Si ndo wahuni wakachoma matairi barabarani sasa gari haziendi wala hazirudi. City Wakaja tena mabomu ya kufa mtuuu. Nikakimbia tena na mtoto mpaka landmark. Yani umo haumo unachezea kichapoo na mabomu unakula vizuri ukizubaa.
Mda huu tunavoongea wahuni wamepora viti, meza matairi wanachoma barabarani, wameenda kuchukua petrol wanataka kuwasha mistimu ya TANESCO kuwe giza totoro vita iwe kamiliiii. Polisi wamekuja wa kutosha na wamejiandaa. Hali ilivo hapa ni tete. Kukiwa giza ndo tutakomaa. Ila vingora vya kutosha vya polisi ndo tunawategemea ila wahuni wameamua kuwa kama vita basi iwe vita.
Kubenea njoo basi uwapooze hawa wahuni ujue. Walikupigia kampeni ujue.