ubungo bus terminal hata hili tumeshindwa?

Rukiko

Senior Member
May 5, 2009
195
57
hiki ni kituo kikubwa sana cha mabasi yaendayo mikoani na hata nje ya nchi ya nchi yetu.
Na kwa utaratibu ulivyo, mabasi huweza kuingia hata usiku wa manane. Na ukifika pale usiku utashaangaa, kituo ni giza sana, kitu ambacho kinaweza kusababisha vitendo vya wizi wa mizigo na au hata ukabaji ndani ya stand yenyewe. Ninaamini kuwa kuna watu wanasimamia kituo kile, je ni kweli kwamba wameshindwa kudhibiti hali ya usalama wa abiria wake na mali zao hasa wanaofika pale usiku pamoja na wapoeaji wao kwa kuweka mataa(mwanga) wa kutosha?
ningeomba pia wasimamizi waboreshe sehemu za abiria kupumzikia hasa pale wanaposubiria kusafiri,au kupokelewa.Michango wanayokusanya pale getini inatosha kuboresha mazingira yote kwa ujumla wake
 
cheki na n mnyika mbunge,huyo jamaa yupo very shap atawa preshalize hao mabwege wa jiji alafu matokeo utayapata tu ndugu.hele inayopatikana hapo kwa siku inatosha kabisa kununua jeneretor la kutoa japo mwanga tu hapo sta.nd
 
Back
Top Bottom