figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,720
- 55,852
Heshima kwenu wakuu,
Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki kuchaguliwa Aprili 4
Kwa mujibu wa kanuni za utaratibu wa uteuzi wa wagombea wa uchaguzi wa nafasi za ubunge katika Bunge la Afrika Mashariki, chama chochote chenye haki ya kusimamisha wagombea kinaweza kuwasilisha wagombea watatu kwa kila nafasi wazi katika makundi yafuatayo:
Kundi A-Wagombea Wanawake
Kundi B-Wagombea wa Zanzibar
Kundi C-Wagombea wa Vyama vya Upinzani
Kundi D-Wagombea wa Tanzania Bara
Mwanachama yoyote atakuwa na sifa za kustahili kugombea na kuchaguliwa kuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki endapo anazo sifa za kustahili kuchaguliwa kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 67 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; si Waziri katika serikali; si mtumishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na ana uzoefu uliothibitishwa au moyo wa kupenda kuimarisha na kuendeleza malengo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Bunge la Afrika Mashariki ni chombo cha Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichoanzishwa chini ya ibara ya 9 ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Mkataba). Bunge hilo linaundwa na wabunge tisa (9) ambao huchaguliwa kutoka kila nchi mwanachama. Aidha, kwa mujibu wa ibara ya 48 (b) ya Mkataba wa bunge hili linajumuisha wabunge wanaoingia kwa nafasi zao (Ex – officio) ambao ni;
a. Mawaziri wanaohusika na masuala ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kutoka kila nchi mwanachama;
b. Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki;
c. Mshauri Mkuu wa Sheria wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hata hivyo, kwa mujibu wa ibara ya 58(2) ya Mkataba wabunge wanaoingia Bungeni kwa nafasi zao hawana haki ya kupiga kura wakati bunge linapopitisha maamuzi yake
UCHAGUZI WA WABUNGE
Kwa mujibu wa ibara ya 50(1) ya Mkataba wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki huchaguliwa na mabunge ya nchi wanachama. Hata hivyo, mtu ambaye ni mbunge katika bunge la nchi mwanachama hawezi kuchaguliwa kuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.
Sifa za mtu kuchaguliwa kuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki zimeainishwa katika ibara ya 50(2)
ya Mkataba kama ifuatavyo;
a. Awe raia wa nchi mwanachama husika;
b. Awe na vigezo vya kumwezesha kuchaguliwa kuwa mbunge katika bunge la nchi yake kwa mujibu wa Katiba ya nchi husika;
c. Asiwe waziri katika nchi mwanachama;
d. Asiwe mtumishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na;
e. Awe na uzoefu na nia ya kuendeleza malengo na madhumuni ya Jumuiya.
Kwa mujibu wa ibara 51(1) ya Mkataba muda wa ubunge katika Bunge la Afrika Mashariki ni miaka mitano (5) ambapo Mbunge anaweza kuchaguliwa tena kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Kwa mujibu wa ibara ya 51(3) mbunge anaweza kuacha kuwa mbunge kama;
a. Atajiuzulu;
b. Atachaguliwa au kuteuliwa kuwa mbunge katika bunge la nchi mwanachama;
c. Atachaguliwa kuwa Waziri katika serikali ya nchi mwanachama;
d. Atakosa kuhudhuria vikao vya bunge kwa kipindi kilichoainishwa kwenye kanuni za bunge; na
e. Akihukumiwa kwa kosa la jinai na kupewa kifungo kinachozidi miezi sita.
MAJUKUMU YA HILI BUNGE LAAFRIKA MASHARIKI NI;
Kwa mujibu wa Ibara ya 49 ya Mkataba, majukumu ya Bunge la Afrika Mashariki ni;
a. Kutunga sheria za Jumuiya;
b. Kuwasiliana na Mabunge ya Nchi Wanachama kuhusu masuala ya Jumuiya;
c. Kujadili na kupitisha bajeti za Jumuiya ya Afrika Mashariki;
d. Kupitia na kujadili taarifa zinazohusu shughuli za Jumuiya, taarifa za mwaka za hesabu za Jumuiya na taarifa nyingine zitakazowasilishwa na Baraza la Mawaziri.
e. Kujadili masuala yote yanoyohusu Jumuiya na kulishauri Baraza la Mawaziri kuhusu:
1. Ajira ya Katibu wa Bunge na watumishi wa Bunge, na
2. Masuala mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa Mkataba.
KWETU TANZANIA UCHAGUZI HUU NI UBABE NA UVUNJAJI KANUNI NDIVYO VINATAWALA
Ibara ya 50 ya mkataba wa kuanzishwa kwa EAC inaelekeza wabunge wapatikane kwa uwiano. Ibara hiyo inaeleza kuwa, Bunge la Taifa kutoka kila nchi mwanachama litachagua wabunge tisa kutoka nje ya wabunge wa bunge husika kuwa wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuzingatia uwiano wa vyama vya siasa, jinsia na makundi mengine.
Mwaka 2012 Tanzania ilicheza figisufigisu ambapo wabunge wengi wa Afika mashriki walitoka CCM kitu ambacho ni kinyume na Ibara ya 50. Nakumbuka aliekuwa Mgombea wa CHADEMA Anthony Komu, alishinda kesi baada ya kulalamikia bao la Mkono la CCMkutozingatia uwiano.
Mwaka huu hii mbinu walioitumia CCM mwaka 2012 haiwezekani tena kwa sababu EALA wanataka uwiano.
My take;
CCM HOFU IMETANDA BUNGENI JUU YA UBUNGE WA AFRIKA MASHARIKI
Habari zinazozagaa mwaka huu ni kwamba kuna uezekano Mkubwa Wabunge wa CCM wakapiga kura za maruhani ili Wabunge wa CCM washindwe ili kuonesha umuhimu wao kwani wabunge wa CCM awamu ya tano wanaalamikia kutokuthaminiwa na kupelekeshwa. Hivyo wanataka kuonesha Hasira zao kwenye Uchaguzi huu ambapo wamepanga kuchagua Wabunge wote wa UKAWA. Kumbuka kura zinapigwa za siri. Wanataka kumuonesha rais kwamba Bunge ni Mhimili unaijitegemea. Hivyowataonesha hasira zao kwenye sanduku la kura.
Baadhi ya hatua ambazo CCM imeanza kuzichukua ili kuepuka dhahama hii ni pamoja na kuwakalisha vikao Wabunge wa CCM na kuwakemea ikiwemo kuwatisha. Hata hivyo tetesi zinadai kwamba, CCM wamepanga kuvuruga utaratibu uliozoeleka wa Kuwapata Wabunge wa Afrika mashariki ili kuondoa aibu. Wanataka Wabunge wa Afika Mashariki kutoka CCM wateuliwe tofauti na Mfumo ulozoeleka wa Kuchagua kwa kupiga kura za Siri mbele ya Bunge, wanahofia kupigiwa kura za maruhani.
SPIKA WA BUNGE NDUGAI AGOMA KUSHIRIKI UOVU NA KUVUNJA UTARATIBU WA UCHAGUZI
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amesema wamekwisha kupokea barua ya kuwataka waanze mchakato wa kupata wabunge na tayari vyama vya siasa vimearifiwa.
“Sisi, kama mambo yote yataenda kama yalivyopangwa, tunatarajia kufanya uchaguzi wa wabunge wa EALA Aprili mwaka huu wakati wa Bunge la Bajeti.
“Muda si mrefu tutakutana kwa ajili ya kufanya makubaliano ili kujua idadi ya wabunge kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wale wa kutoka Upinzani. Tanzania ina nafasi tisa na zinatakiwa kuzingatia vyama, jinsia na Muungano” alisema Ndugai. Bado imekuwa Vigumu kumshawishi Ndugai afanye kama wanamkakati wa CCM wanavyotaka.
WABUNGE WALIOMALIZA MUDA WAO AMBAO WANAWEZA KUGOMBEA TENA NI;
Charles Makongoro Nyerere
Issa Twaha Taslima
Abdullah Ally Hassan Mwinyi
Shy-Rose Sadrudin Bhanji
Adam Omar Kimbisa
Angela Charles Kizigha
Bernard Musomi Murunya
Perpetua Kessy Nderakindo
Maryam Ussi Yahya
VIJANA WENGI KUJITOSA KWENYE UCHAGUZI HUU
Tayari vijana wa Vyama vyote waliowengi wanaulilia uchaguzi huu wa Afrika Mashariki
Kwa Upande wa CCM Machali yupo Tayari, Dkt. Said Gharib Bilal yupo tayari, Sofia Ali Rijaal yupo tayari na Khamis Jabir Makame William John Malecela Nk.
UKAWA naona Kafulila kadhamilia, Lwanyantika Masha, Mwaiseje S. Polisya, Nusrat Hanje, Wema Sepetu nk.
Je, watu gani unapendekeza wawakilishe nchi EALA?
Nani unamfahamu anautaka huu Ubunge? Je ana vigezo na uwezo wa kutetea Nchi kwa Mambo Muhimu ya Kitaifa bila kuingiza Uchama?
USHAURI WANGU
i) Tutangulize Tanzania mbele sio vyama vyetu. Tusikomoane wala kulipizana visasi. Tumtangulize Mungu Mbele. Sisi wote ni Watanzania, kwanini tugombanie fito wakati twajenga nyumba moja?
ii) Tufuate kanuni na taratibu za Uchaguzi zilizowekwa kikatiba badala ya Ubabe na Tamaa.
*Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
1. Ee Mungu twakuomba uilinde Jumuiya Afrika Mashariki
Tuwezeshe kuishi kwa amani Tutimize na malengo yetu.
Jumuiya yetu sote tuilinde Tuwajibike tuimarike Umoja wetu ni nguzo yetu Idumu Jumuiya yetu.
2. Uzalendo pia mshikamano Viwe msingi wa Umoja wetu Natulinde Uhuru na Amani
Mila zetu na desturi zetu.
3. Viwandani na hata mashambani Tufanye kazi sote kwa makini
Tujitoe kwa hali na mali Tuijenge Jumuiya bora.
Habari zaidi...
Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki kuchaguliwa Aprili 4
Dodoma. Uchaguzi wa Wajumbe Tisa (9) watakaoiwakilisha Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA) unatarajiwa kufanyika katika Mkutano wa Saba wa Bunge unaotarajiwa kuanza Aprili 4 mwaka huu.
Uchaguzi huo utakaofanyika Dodoma, utazingatia maisha ya bunge hilo lililoingia madarakani mwaka 2012 ambalo litafikia ukomo wake Juni 4 mwaka huu.
Taarifa iliyoletwa kwa vyombo vya habari na Kitengo cha Bunge cha Habari, Elimu na Mawasiliano imeeleza kuwa uchaguzi huo utasimamiwa na Katibu wa Bunge ambaye atatoa tangazo kwenye gazeti la serikali la kesho.
“Katibu wa Bunge atatoa tangazo kwenye Gazeti la Serikali kesho tarehe 17 Machi, 2017 linaloainisha siku ya uteuzi wa wagombea kuwa tarehe 30 Machi, 2017 saa kumi kamili jioni na siku ya uchaguzi kuwa ni tarehe 4 Aprili, 2017 mara baada ya kipindi cha maswali na majibu Bungeni.” Ilisema taarifa hiyo
Katika taarifa hiyo, msimamizi wa uchaguzi alitoa wito kwa Watanzania wenye sifa za kugombea na kuchaguliwa wajitokeze.