Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
UBUNGE ni sehemu muhimu sana ya maisha ya Watanzania kwani inaleta maana halisi ya demokrasia.
Wabunge huchaguliwa na wananchi ili wakazungumze kwa niaba yao hivyo hatuwezi kupuuza umuhimu wa wajumbe hawa kwani wamebeba dhamana kubwa ya Watanzania nyuma yao.
Kutokana na umuhimu wa wajumbe hawa ni muhimu tukapeleka wajumbe walio bora waende kujenga hoja zenye tija kwa taifa na hususan kwa wananchi wao waliowachagua.
Miongoni mwa vigezo vilivyowekwa kuwapata wajumbe hawa ni pamoja na kuwa na akili timamu, awe raia wa Tanzania, atokane na chama cha siasa, awe na umri wa miaka kumi na nane na kuendelea na ajue kusoma na kuandika. Haya yote ni kwa mujibu wa Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Soma zaidi hapa=> Ubunge ni zaidi ya kujua kusoma na kuandika | Fikra Pevu