Ubunge East Afrika: James Milya anatufaa!!

Ubunge East Afrika: James Milya anatufaa!!

mi nikishaona mrisho tu,naona ni afadhali tusiwe na mwakilishi

Mkuu Nyalotsi, Umeona ee!! Huyu Mrisho GAMBA, ni KIMEO.......hafai kusema ukweli....kwa watu wanaomfahamu huyu mtoto ni dhahiri sio mtu wa kupewa hata balozi wa nyumba kumi2!!
 
Huyo namba 6 mrisho gambo binafsi namwona ni mzuri zaidi kweli kwa upeo alio nao

Upeo upi? Fafanua! Lete historia yake (CV) tujiridhishe na huyo Gamba wako!!
 
Yupo kundi gani la lowassa or? Halafu cjakuelewa unaposema ana huba unamaanisha nn?

Kundi la Watanzania wazalendo!! Tumpe support nawahakikishia watz hamtojilaumu katika kumpatia huyu Millya nafasi hii...kila mmoja atimize wajibu wake kwa kumshawishi Mbunge wake ampatie kijana huyu kura yake!!
 
wana jf,

kwa kutambua unyeti wa nafasi hii ya uwakilishi katika bunge la afrika mashariki; naomba tujielekeze katika uhalisia na sio hisia au siasa zenye chuki!! Miongoni mwa vijana wetu waliojitokeza kutangaza nia ya kugombea nafasi hiyo ni mwenyekiti wa uvccm mkoa wa arusha mh. James kinyasi millya.

Huyu kijana ana sifa zifuatazo:

1. Ni msomi, mwenye degree ya sheria (llb) tumaini university-iringa
2. Alikuwa rais wa chuo hicho-aliaminika katika hoja na kutetea haki na maslahi ya wengi.
3. Ana masters ya sheria pretoria university-south africa
4. Ana uzoefu mkubwa katika kufanyakazi ndani na nje ya nchi
5. Akiwa intern ya sheria katika mahakama ya ictr pale arushakama mwanafunzi wa pretoria univrsty;
alichaguliwa kuwa rais wa wanafunzi (interns) katika mahakama hiyo!
6. Ni kijana mzalendo, mnyenyekevu, mwenye huba, busara, hekma na heshma kwa watu wote
7. Ni mjumbe wa baraza la vijana la utekelezaji uvccm taifa
8. Ni mwenyekiti wa uvccm mkoa wa arusha
9. Mjumbe wa kamati kuu ya ccm mkoa wa arusha
10.ni kijana mwenye maono na mzalendo mwenye kupenda nchi yake mfano wa sokoine na baba wa
taifa mwl.nyerere!

Kwa haya machache na ninaamini wengi wa wana jf wamekuwa wakimuunga mkono kijana huyu, basi tuendeleze mshikamano wetu na uzalendo katika kuwapata vijana wazalendo wenye kiu ya maendeleo kwa nchi yetu!! Kila mmoja atimize wajibu wake kumuunga millya mkono ili hatimaye atuwakilishe katika bunge letu la ea!!

Mungu ibariki afrika, mungu ibariki tanzania!!!

nawasilisha!!!

lowassa!!lowassa!!!lowassa!!!!
 
Back
Top Bottom