Ubovu wa huduma Benki ya NBC Arusha

Ubovu wa huduma Benki ya NBC Arusha

Jamani sijui tu NBC inapitia masahibu gani, inaskitisha kwa kweli. Na tatizo kubwa ni wafanyakazi wake. Yani hawana habari na wateja kabisaaa. Hata ulalamike vipi unadharaulika tu. Hiyo ya Arusha ni majanga kwa kweli, yashanikuta mengi hapo. Ukiingia usahau habari ya muda. Unaweza kumpasua mtu kwa hasira. Na manager wao huwa yupo. Sijui huwa haoni! Headquarters ya hii bank ifanyie kazi haya malalamiko ya wateja. It's just too much
 
Tellers nao wengi wazee,foleni watu 7 ila inachukua masaa 3 kumfikia
 
Pesa yangu imenasa kwenye transactions za bank account na tigo pesa toka mwezi wa 9 hadi leo wananizungusha. Njoo leo njoo kesho.

Hii mambo kama sio very urgent usifanye system haiko reliable hata kidogo.
 
Pale Arusha Meru Branch nimefatilia kujiunga internet banking na fomu nilijaza mpaka sasa zaidi ya miezi minne haijawa tayari. Mara wanasema mtandao haupo vizuri, mara muhusika ametoka na lazima awe yeye mwenyewe, yani kila siku hawakosi sababu. Hivi hawa watu wapo makini kweli?
 
Nawashauri mhame hiyo bank.Exim bank tawi la kariakoo walinisumbua pale kuchukua kadi yangu ya atm nikahama.Huwa sina uvumilivu na bank zisizoendeshwa kitaalam(zinazokosa weledi) kabisa.
 
Sina hamu na hii Bank, nilikuwa kampuni flan kila mwisho wa mwez tunalipwa kwa cheki NBC, ilikuwa ukienda sa nne kutoka nao jion. Wako slow sana stak hata kuwaskia.
 
Back
Top Bottom