Ubovu wa huduma Benki ya NBC Arusha

Ubovu wa huduma Benki ya NBC Arusha

mabwepand

Member
Joined
Jul 16, 2012
Posts
86
Reaction score
22
Hii bank sijui inaelekea wapi kwani huduma zake ni mbovu mbovu kabisa kuliko bank yoyote ile niliyowahi kwenda katika nchi hii ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nilichoshuhudia pale dawati la huduma kwa wateja customer care hakuna huduma bali ni kero kwa wateja. Please badilikeni tafadhali sana, imagine mtu anakuja kutaka huduma au ufafanuzi wa jambo ambalo kwa kawaida haliwezi chukua hata five minutes unawekwa pale for about 5 hours.

Hii bank sijui ipo serikalini au binafsi, please management ya NBC BANK ARUSHA na makao makuu tupieni jicho NBC makao makuu Arusha.

Wafanyakazi kazi kujizungusha, sijui ni umri umewatupa mkono au!!

JIREKEBISHENI mteja ni mfalme hela zangu zina bank charges nawe ndio unalipwa kupitia kwangu na mikopo mnayotoa kwetu.
 
weka ela mchagoni mr
kw nini wakuangaishe na ela yako
 
Hawa jamaa hawa mmh, we ngoja uone kama watarekebisha!!,pamoja na kupata hiyo taarifa, lkn kuliondoa tatizo kwao ni majanga.
 
Hii bank nadhani ni ya watoto wa vigogo au wafanyakazi wote wana hisa kwani wana madharau na wanahudumia kama hawataki utadhani hawalipwi, sijui hata uongozi wao hawaoni ili wawasaidie wateja wao?
 
Hii bank sijui inaelekea wapi kwani huduma zake ni mbovu mbovu kabisa kuliko bank yoyote ile niliyowahi kwenda katika nchi hii ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nilichoshuhudia pale dawati la huduma kwa wateja customer care hakuna huduma bali ni kero kwa wateja. Please badilikeni tafadhali sana, imagine mtu anakuja kutaka huduma au ufafanuzi wa jambo ambalo kwa kawaida haliwezi chukua hata five minutes unawekwa pale for about 5 hours.

Hii bank sijui ipo serikalini au binafsi, please management ya NBC BANK ARUSHA na makao makuu tupieni jicho NBC makao makuu Arusha.

Wafanyakazi kazi kujizungusha, sijui ni umri umewatupa mkono au!!

JIREKEBISHENI mteja ni mfalme hela zangu zina bank charges nawe ndio unalipwa kupitia kwangu na mikopo mnayotoa kwetu.

ukija huku tawi moro utagundua huko Arusha bado mko vizuri.... yaani kitu ambacho wako makini nacho ni muda wa kufunga
 
  • Thanks
Reactions: amu
Juzi nilikuwa nbc ubungo.....niliingia saa saba nikatoka saa 10 sababu ya foreni!!!! Poor nbc!! Harafu kuna teller yule wa dirisha number 1 hana adabu kabisa!
 
hâta Dodoma Huduma za NBC haziridhishi kuweka tu pesa unatakiwa utenge siku nzima
 
Pesa yangu imenasa kwenye transactions za bank account na tigo pesa toka mwezi wa 9 hadi leo wananizungusha. Njoo leo njoo kesho.
 
Nbc nayo ni bank? Mimi niliwahama mapema sana ni kichefuchefu.
Walivyohamia hapo kwenye jengo la megacoplex ndio wakawa hovyo kabisa.
 
Mimi nilishafunga account yangu hapo siku nyingi.

Hakuna siku iliyonikera na ikapelekea mie kuachana na NBC ni siku ambayo nilienda kudraw pesa zangu tawi la MZA hapo mtaa wa liberty, ambapo mhudumu aliniona siwezi miliki kiasi hicho cha pesa kweli nilifika saa 4 ila niliondoka saa 10 mpk wateja wote waliondoka na nilipokuwa nawasikiliza wanawasiliana na wenzao Dodoma nilipofungulia akaunti wanazungumza eti mwenyewe alivyo.hawezi miliki, na ingawa walishatuma FAX bd walinisumbua toka siku hy nilitoa pesa zote na sikurudi tena
 
  • Thanks
Reactions: amu
Hii Benki ilishauzwa, kwa hiyo nadhani Morali ya wafanyakazi ipo chini sana
 
Basi huyo mmiliki mpya ndiye tatizo. Kama hawezi kuendesha bank, aachane na biashara hii kuliko ku frustrate wateja pasipo sababu!.

Kwenye soko "holela" ooops "huria" mteja hatakiwi kuwa "frustrated" na "mfanyabiashara" - Benki zipo nyingi sana hapa Tanzania kwa sasa...!
 
Sasa ifungwe ili watu tutafute options zingine za kupata huduma hiyo. Watu walifungua Accounts zao NBC. Watu binafsina Mashirikai pia. Leo ghafla bank inawanunia na kuwapa huduma za ovyo hujaawahi kuona bank yoyote.
Lazima itafrustrate.

Wakitangaza kufunga, watu watajiandaa kuhamisha fedha zao na kuzitafutia namna nyingine.

Nilienda NBC tawi moja. Kwa dakika 20, teller windows 3, zikawa zimehudumia watu 4. Kila dakika folleni imejaa. Hata ukikukta watu 10 mbele yako, tegemea kutoka baada ya muda usiopungua lisaa limoja. Swali ni network iko chini, au ni upolepole wa wahudumu ambao hawajali muda wa wateja?

Ninashangazwa na upolepole wa tellers wa NBC, wanafanya kazi kama vinyonga sasa haijulikani kama wanafanyaga hivyo wakijua hata akifanya haraka, itabidi akae idle akisubiri mtandao urespond, au taratibu hiyo hiyo ndiyo inayofanya wachelewa hata ku comand processes za computer?

Honestly NBC ni kifo!.

Kwenye soko "holela" ooops "huria" mteja hatakiwi kuwa "frustrated" na "mfanyabiashara" - Benki zipo nyingi sana hapa Tanzania kwa sasa...!
 
Siku hizi fedha tunaweka kwenye vicoba tofauti tofauti
 
mimi imenichosha kabisa,atm pale philips ilimeza kadi yangu nikaenda pale nbc wakaniambia nirudi baada ya wiki nikawaambia nasafiri wakaniambia baada ya wiki kupita wataiharibu nikirudi nitoe elfu kumi nipatiwe nyingine.
halafu benk yoyote unayoingia unakuta wastani wa umri ni 45 ujue ni majanga.
 
Naomba kwa wenye kuifahamu vicoba vizuri kuhusu utaratibu Wa kukopa online.napata wasiwasi kutuma hela kwa mpesa zawadi walizohainisha pia zinanipa utata.isijekua ni kama Desi
 
Niwezi pia wa pesa yako uliyoweka katika account yako
 
Back
Top Bottom