Kwa kipindi cha takribani miezi miwili, kumekuwa na maji ya kilimanjaro yenye chumvi tofauti na kilimanjaro iliyozoeleka.
Najua watumiaji wa maji haya tu wengi, ikiwa ni watu binafsi na taasisi binafsi na za umma. Vikao, mikutano na hafla zote muhimu huwezi kukuta maji tofauti na kilimanjaro.
Na ukweli usiopingika kwamba, hali hii inatokana na ubora wa maji haya pendwa ya kilimanjaro. Lakini ninachelea kusema kwamba kumbe ni kweli mgema akisifiwa tembo hulitia maji. Kama haya maji yanazalishwa na Bonite bottlers, basi kampuni inatakiwa itoe maelezo kwa wateja wake kuhusu chanzo halisi cha maji haya badala ya kutuandikia Shirimatunda ilhali yanonyesha ni ya kisima.
Na kama kuna uchakachuaji pahala basi kampuni itoe tamko ili kuwalinda watumiaji wa maji haya.
Ninajua humu jukwaani hawawezi kukosekana watu wa kampuni. Na nimeliweka hapa baada ya kutopata namna ya kuwasilisha malalamiko kwa kampuni kwani, kwenye chupa kuna sanduku la posta tu. Hakuna email wala namba ya simu.
Kazi njema.