ubora wa elimu na usimamizi wake

The golden

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
1,381
2,553
Wakuu heshima kwenu;

Tumejidanganya kwa mda mrefu sana, na tunaendelea kujidanya kuwa ,matumizi ya vitisho ,lugha za kejeli na kuwabeza walimu vinaweza kutusaidia katika harakati zetu za kuboresha elimu.

Linapotokea tatizo la watoto kushindwa mitihani yao ,walimu na viongozi wengine wa kada hii wamekuwa wakitupiwa lawama zisizobebeka. Hii si sawa hata kidogo. Tumeacha kushughulikia matitizo ya msingi yalipo kwenye sekta hii tumebaki kuwalaumu walimu tu, walimu ambao ukifanya mazungumzo nao ya karibu utagundua kuwa wengi wamekata tamaa, hawana tena matumaini ndoto zao zimezimwa kabisa na mazingira duni ya kazi hii. Wachache wamejiingiza hata katika dibwi la unywaji wa pombe za kienyeji huko vijijini. Huku wakiwatambia walevi wenzao kuwa wao ni wasomi kutoka vyuo vikuu.Hii ni aibu.

Leo hii huwezi kufahamu walimu wanawajibika kwa nani. Sasa hivi kila kiongozi amekuwa mamlaka ya nidhamu kwa walimu.Wanasiasa hata wasio na taaluma yoyote wamekuwa ma-boss wa walimu. Kila mtu anayetaka kutafuta umaarufu wa kisiasa amekuwa akiitumia kada hii kutimiza malengo yake. Hii ni aibu kwa taifa.

Tukicheza na elimu ,tunacheza na faifa. Taifa la watu makini huandaliwa shuleni.Watu makini hawawezi kupuuza elimu. Kupuuza elimu ni kujiandaa kuwa watumwa badae.Watu wasio na maarifa ya kutosha hutawaliwa na wenye maarifa.

Naomba tubadilike , tuanze kuwathamini walimu na kuwapa heshima hawa ndio wanaoandaa taifa la badae.Tuwekeze rasilimali zetu katika elimu ili tupate rasilimali watu watakaoisaidia nchi.
 
Back
Top Bottom