Ni sahihi kabisa mkuu open university unajua tu mwaka wa kuanza masomo ila mwaka wa kumaliza hauwezi jua hata kidogo! kama kuna mtu anabisha ajaribu kujiunga.Sijui kama ni kweli au si kweli. Ila ninachokifahamu Waliosoma Open University kwenye soko la ajira au hata kwenye udahili wa vyuo vingine, vyeti vyao vinaaminika zaidi kuliko vyuo vingine (kama Udom).
Lakini ili umalize Open University ni Muhimu "ukaagana na nyonga".
Dondoka simama, dondoka simama ni nyingi. Ni moja ya vyuo vigumu sana kusoma. ukifanya uzembe uzembe unaweza soma hata miaka 6 bila ya kumaliza degree.
ukitaka degree ya chap chap usiende Open University hakunaga hizo.
NB: Ni moja ya Vyuo bora Tanzania. Kipo kwenye top 5 best university of Tanzania.
Somo hili Ndalichako na JPM (na wengine wengi hapa JF) hawataki kulielewa kabisa. Tusubiri awamu nyingine kwani hata foundation courses waliisimamisha labda kama watalegeza kamba baada ya OUT kupeleka maombi kwa wahusika. Kwa sasa open university sio open kinadharia ni jina tu."Huria" kwenye Chuo Kikuu Huria (OUT) maana yake mtu yeyote anaweza kusoma hapo. Ila kila mtu anatoka na cheti kinachoonyesha uwezo wake (cheti, diploma, digrii, n.k.). Kimsingi uhuria wa OUT ndio sifa yake kubwa inayopaswa kulindwa. IMHO, ni mapungufu makubwa kulazimisha OUT itumie vigezo vya udahili vinavyotumiwa na vyuo vingine visivyo huria.
Na pia waliosoma OUT na wakawa na namna ya kulinganisha na vyuo vingine, aghalabu hukisifia sana Chuo Kikuu Huria.
Open wako vizuri tu. Kuna wakati UDSM walianza kubagua (GPA za vyuo tofauti) kwenye post graduate admission criteria lakini sasa naona wameacha. Kwenye kazi inawezekana watu wakabagua kimya kimya. Kazini pia kuna old-boys networks hasa kama panel ya usaili haiko balanced hizi zinaweza kubagua kutokana na hisia au upendeleo.Mtu aliyepata shahada yenye GPA ya 3.5 ya Open yuko vizuri zaidi kuliko yule aliyepata GPA ya 3.5 vyuo vingine,? naomba kufahamu hilo!
Somo hili Ndalichako na JPM (na wengine wengi hapa JF) hawataki kulielewa kabisa. Tusubiri awamu nyingine kwani hata foundation courses waliisimamisha labda kama watalegeza kamba baada ya OUT kupeleka maombi kwa wahusika. Kwa sasa open university sio openkinadhariakihalisia ni jina tu.