The hammer
JF-Expert Member
- May 17, 2011
- 2,381
- 1,760
1:Vicent Angban
Anaweza kupanga safu yake ya ulinzi vizuri.Ni goalkeeper ambaye hajawahi kupata kashi kashi yoyote ambayo inaweza kumpima uwezo wake.Ingekuwa si uimara wa safu ya ulinzi wa Simba,basi huyu goalkeeper angekuwa ndo kipa mbovu kuliko wote katika msimu wa ligi kuu Tz bara.Kimo chake kinamfanya mipira inayotambaa chini kuwa tabu kwake na upana wa goli haukadirii ipasavyo.
2:Bokungu.
Ni mchezaji imara na anajua kukaba vyema na kulinda upande wake usiwe chanzo cha matatizo langoni mwake.Tatizo lake hana mbio sana na hivyo hawezi kupandisha mashambuli ipasavyo.Tatizo hilo limetatuliwa kwa kuwepo kichuya ambaye ana mbio na anauwezo wa kumiliki mpira katika winga ambayo alitakiwa Bokungu kusaidia team inaposhambulia.
3:Mohamed Hussein.
Ni mlinzi anayejituma sana,ana control nzuri ya mpira na ana mbio kiasi.Tatizo lake anapopiga mpira iwe cross,kona au foul hanyanyui mpira juu kiasi kwa kama ni kona,foul au cross basi mipira mingi inaishia kwa mlinzi wa kwanza tu.Pia ana tabia akipata mpira ana nyanyua kichwa juu akiwa anaangalia mahali pa kupeleka mpira,yes ni sahihi lakini inakuwa sahihi sana iwapo upo nyuma sehemu kama mita 18 na hakuna adui ila si katikati ya uwanja na mara kwa mara ananyang'anywa mpira kwa style hii.
4:Mwanjali
Anaweza na ni mlizi mzuri(Kasoro zake sijazitambua bado)
5:Murshid
Ni mlinzi mzuri na wa kutumainiwa sana,anajua kukaba na anashambulia pia pale team inapopoteza matumaini ya kurudisha goli.Tatizo lake anacheza madhambi sana kiasi kwamba mnaweza kufanya sub isiyopangwa kwa kuogopa red card.
6:Mkude
Amekuwa nguzo muhimu pale katikati ana control na anajuwa kugawa mipira.
7:Kichuya.
Ana kasi na ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira,ana kasi na anajua kupiga mipira ikalenga goal.Sijaona tatizo lake sana.
8: Mzamiru Yassin
Ana uwezo wa kuchezesha team na kugawa mipra ipasavyo.Tatizo lake pasi zake wakati mwingine ni za hovyo na zisizo na macho.
9:Mavugo
Huyu sasa amekuwa kama wale nyoka wasio na madhara.Mashabiki walikuwa na matumaini makubwa sana kuliko Okwi ila sasa imekuwa tofauti.Anajua kuuchezea mpira na kuumiliki ila inapofikia hatua ya yeye kugawa mpira kwa mtu aliyeko katika nafasi ya kufunga ndipo utakapoona vioja..ni mchoyo sana na anajali matokeo yake yeye kuliko ya team,na hii ni kutokana na alichofikiria ni tofauti na anayoyakuta field ni kama vile student anasoma UDSM then anawaza akihitimu tu atapata ajira na mwaka mmoja kazini atakuwa na nyumba,gari na mtoto mkali ndani but akiwa fueld sasa miaka 4 no ajira no money unafikiri nini kinatokea.
10:Ajib
Ni mshambuliaji mzuri,anajua kuuchezea mpira na kuhadaa walinzi na kutoa pasi.
11: Kazimoto
Anajitahidi sana na anajua kuchezesha team na kugawa mipira.Tatizo anachoka hasa kipindi cha pili na anahitaji awe na msaidizi sio wa kumaliza dk 90 hii ni kutokana umri unakaribia kufikia tamati katika mchezo wa mpira wa miguu.
Sub
1:Manyika
Ni mzuri kuliko Angban ila hajapewa nafasi labda kuna sababu kadhaa za kinidhamu.
2:Lufunga
Ni mzuri ila timing ya kukaba inamsumbua hivyo Murushid atabaki kuwa bora zaidi kuliko Lufunga.
3:Blagnon
Ana uwezo mzuri hata kuliko Mavugo ila bado hajajiamini tu katika ligi ya Tz.