Ubora na changamoto za UDOM -Chuo Kikuu cha Dodoma

Ubora na changamoto za UDOM -Chuo Kikuu cha Dodoma

qnizxy

Member
Joined
Jul 18, 2017
Posts
5
Reaction score
1
Uzi huu ni maalumu kuelezea ubora na changamoto za Chuo kikuu cha Dodoma.
Kwa maswali haya machache nahisi tutaibua hoja nyingi za msingi na sio mabishano ya chuo kipi bora.
-Yapi mafanikio ya Chuo kikuu cha Dodoma?
-Zipi changamoto za chuo kikuu cha Dodoma?
-Je, products za Udom zinafanya vizuri makazini ? zina soko?
-Kwanini wanakiita Udom chuo cha kata??
-Kuna ukweli wowote kuwa Udom ni vilaza? Kwa hoja zipi?

Mada mezani...mabishano hayajengi, hoja zinajenga na kuelimisha.
KARIBUNI kuchangia.
 
Ngoja nitoke nje ya mada.
Hiki chuo kina kama miaka miwili hakiajiri wahadhiri.
Ni vipi?
Au wanapeana ndugu kwa ndugu na sisi wengine tukatafute ndugu pale??
 
Wengi tutakaocomment hapa ni wale wa elimu za hapa na pale. Kufika chuo labda kujiunga bando au kutembelea ndugu na marafiki. Usitegemee sana mchango wa maana hapa. Jaribu kutembelea website Yao pia research direct kwa alumni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa hakuna cha zaid ya mapishano tuu na kejeli..
Bado cjaona dhumun la post yako
 
Chuo huwa hatutaki stress za maisha, na chuo Pekee cha kuweza kukufanya uyafurahie maisha ya chuo na elimu yako ije kuwa na manufaa katika mazingira halisia ni UDOM. kama unataka sifa na kujidai mitaani nenda Mlimani ( wanajiita Vipanga, Harvard n.k)
 
kwanza napenda kusema kuwa tusiwe na matabaka katika swala la elimu ya juu huwezi kusema kuwa labda chuo fulami kwakuwa kinasifika basi kila wahutimu wanaotoka halo wanaingia kwwnye ajira direct hiyo kauli sio kweli swala la kuajiriwa haiangalii chuo gani umetoka na una GPA kiasi gani kushimda wenzako hasa linapokuja kwenye issue za interview..interview nyingi wanaangalia confidence, capacity ya mtu kuelewa vitu, memorization ya vitu ulivyovipitia hasa kwenye field ulizofanya, na maswali mengine ya kukupima ambayo yanakuwa very logic...
MM ni muhitumu wa UDOM Kwa mwaka 2016/2017 holder of bachelor of science in chemistry in a college of natural and mathematical sciences...actually changamoto zipo mfano maabara kwa sasa hazijitoshelezi lakini kwa muhula unaokuja maabara itajitosheleza na kwani vifaa vya analysis ambavyo vipo more advanced vipo njiani kuja...lakini ukiachilia hiyo system ya uongozi was chuo unatesa sana wanafunzi kwani unapopata tatizo ukitegemea chuo utaumia,, watu wanazungumza kuwa UDOM kuna shida ya maji mm binafsi kwa miaka yangu mitatu naona hakuna shida ya maji, maji huwa yanatoka Ila sisi wanafunzi tunataka kuona maji yanaflow hadi ndani kila muda tunasahau kuwa kule vyanzo vya maji ni visimani, ukijiingeza kwa kununua majaba, ndoo na madumu huwezi kusema kuwa unashida na maji Ila ukikaa usubirie muda was kutaka kutumia maji ndo uende kuchota lazima utazungumza kuwa udom kuna shida ya maji. licha ya kukumbana na changamoto nyingi lakini nafurahi kuhitimu katika chuo cha UDOM kwani kwa kile nilichokipata natumaini kitanisaidia kwa maisha ninayoenda kuyakumbana nayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UDOM ya mwaka 2007-2010 sio ya 2017 kuna mabadiliko mengi yamefanyika ikiwemo vifaa vya kufundishia, maabara wfahadhiri wa kutosha!! hata wahitimu wake wa sasa wamefanikiwa kuleta ushindani kwenye soko la ajira!!! Uwepo wa hospital ya BWM Kumeleta mapinduzi katika utoaji wa wahitimu bora kwenye fani ya afya.
 
ukiongelea Udom utakuwa unaongelea chuo kikubwa Africa maahariki na kati pamoja na ukubwa vchangamoto vipo maana ukiangalia enrollment ni kubwa ukicompare na vyuo vingine
Udom ni chuo kizuri sijapata ona na product zake znasifika kuwa na nizamu ya hali ya juu huku makazini hasa ukimpata mwalimu aliyetoka udom ni mwalimu kweli hawanaga longolongo

hiki chuo nakipenda kwa kitu kimoja kikubwa walimu na watawala Wa pale wapo makini na uwezo Wa mtu ukionesha unaweza na ukathamini mchango wao watakufikisha mbali kadri ya uwezo wako, ila ukijitoa ufahamu ukajifanya kuelimika ni kumeza module tu wapo wanajua pia kukumezesha module

kiukweli hakuna chuo kizuri kama udom kuanzia mazingira mpaka miundo mbinu japo sisi wanafunzi tunashiriki kuhiharibu

kwa wanaoendelea na wengine tunaojiunga tafafhali tukitunze hiki chuo
 
Mkuu qnizxy

Nimepita hapo muda hivyo naamini mambo mengi yanaweza kuwa sivyo yalivyo leo, kwa uchache strength ya Udom wakati uko chuoni ni malazi, nadhani ndio chuo pekee bongo ambacho mwanafunzi anaweza kuwa na uhakika na malazi kwa miaka yake yote atayokuwa chuoni. Pili mazingira mazuri ya kusoma, chuo kimejitenga na kina majengo ya kutosha kwa ajili ya madarasa kwa kujisomea au kufanya chochote bila kuhangaika na venue.

Kitaaluma, wakati nipo kuna baadhi ya college kweli zilikuwa shida kwa njia moja au nyingine(Kila college ina kautawala kake) lakini watu wa Informatics na walimu walikuwa makini sana na wanachofanya na hata baada ya kutoka chuo sifa zao zinasikika sijui sasa labda na wengine wameunga. Pia kuna baadhi zilikuwa matatizo kama watu wa biashara.

Udhaifu wa Udom ilikuwa maji aisee, ni shida, kuanzia ya kunywa mpaka ya matumizi mengine. Maji yalikuwa na ladha ambayo wengi hawakuipenda hivyo kuna bajeti ya kununua maji maisha yako yote chuoni labda uridhike nayo, pili maji kwa ujumla ni tatizo hasa chuo cha walimu, social sciences na humanities angalau(Nimeishi hivyo viwili).

Udom kuitwa chuo cha kata nadhani ni just a myth, labda mwanzo watu wenye vigezo hafifu waliweza kudahiliwa hasa walikuwa wanalinganisha na UD au kuchukua wanafunzi wengi etc lakini all in all Udom ni chuo bora kuliko vyuo vingi sana nchini.

Mwisho kwa mawazo yangu, chuoni is about mhusika hasa chuo ambacho kimejumuisha kada nyingi tofauti na watu wengi wenye utaalamu tofauti. Ni sehemu pekee ambao unaweza kujifunza vitu unavyopenda/unavyohitaji kwa gharama nafuu au bure na kuwa mhitimu bora baadae ukizingatia muda loose chuoni ni mkubwa sana, mimi nafanya kitu tofauti na nilichosomea kitaaluma na nilijifunzia chuoni kwani wakati naanza chuo nilikuwa mweupe sana kwenye upande huo, kupitia marafiki na kupenda kujua nimekuwa bora sana bila kutoa hata senti tano na naamini nafanya vizuri kuliko hata baadhi ya waliosomea.

NB: Miaka mingi imepita na nimetaja vitu angalau nilikuwa na ufahamu navyo au vilinihusu, unaweza kutafiti upya.
 
Back
Top Bottom