Ubishoo mwingine bwana..soo!!

Ubishoo mwingine bwana..soo!!

Shukuru

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2007
Posts
747
Reaction score
16
Brothermen mmoja aliyekuwa akijifanya anajua ung’eng’e huku akijifanya yeye ni matawi ya juu alikwenda kupata msosi yeye na demu wake.Si unajua mabishoo kwa kupenda kujikweza? Basi demu akaagiza chipsi kuku jamaa akaagiza wali nyama.

Baada ya kumaliza wakaletewa bili yao ambayo ilikuwa ni sh, elfu (15,000). Kumbe jamaa mfukoni alikuwa na kiasi hicho hicho cha pesa, akalipa lakini kwa shingo upande huku akimuomba Mungu yule demu asijekuagiza kitu kingine maana ataumbuka.

Ile wanainuka tu demu si akamuomba mhudumu amletee ‘tooth stick’ za kuchokonolea meno ambazo hutolewa bure kwa mteja. Yule brothermen kusikia vile akaanza kuwaka akijua kwamba atatakiwa kulipa wakati hana kitu mfukoni na kuwaka akisema “Sweet yaani unaagiza tena? Hizo ‘tooth stick’ utalipa mwenyewe” Demu kusikia vile akajua jamaa kumbe hakwenda hata darasa moja! Palepale kila mtu akashika njia yake...
 
Kumbe kutokujua lugha kunaweza sababisha 'divorce!'
 
Mwanzoni, wanaume tunaji-sacrifice sana kwa wadada. Baadae mambo hugeuka. Y?????
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom