Ubinasi wetu ndo tatizo la ajira!!!!!!!!!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubinasi wetu ndo tatizo la ajira!!!!!!!!!!!!!!!

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by msani, Sep 4, 2011.

 1. msani

  msani JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Kila unaposoma post za watu kilio chetu kinafanana.......ajira.....ajira....ajira....
  Lakini wana jf mi nadhani tumekuwa wabinafsi sana na hatutaki kushirikiana,ni ukweli kwamba hatuna mitaji lakini kuna kazi zingine hazihitaji mitaji kwani kile ulichonacho kichwani ambacho umesomea miaka 3 au hata zaidi ni mtaji tosha iwapo mkikubali kushirikiana na wenzako,...watu hawataki kujiunga pamoja na kuanzisha ofisi yao ambapo kwao mtaji ni akili zao ambazo ni hitaji kubwa kwa jamii na badala yake tunalilia kuajiriwa tu ili tuendelee kuwa maskini na kuwanufaisha wengine kwa msoto ambao tumeusotea wkt tunasoma.
  Kuanzisha kampuni yako kweli kuna msoto lakini mshindo wa mafanikio yake hapo baadae ni mkubwa.tunadanganywa kuwa kuna benki ya vijana inaanzishwa ambapo tunaweza kuanzisha biashara zetu lakini hao vijana wanaoongelea huenda usiwe wewe kwani huenda ukawa haupo ktk chama fulani cha siasa kwa hiyo msoto wako utakuwa palepale.mi nawaasa vijana wenzangu tujaribu kujiunga na wenzetu wa fani tofauti tofauti ili tuanze kuuza utalaamu wetu kwa jamii na tusisubiri mambo mepesi mepesi tu.
  Najua vijana wengi mtachukia kwa ujumbe huu lakini ndio ukweli kwa mafanikio yako.
  Mi nimemaliza chuo mwaka huu lakini tangu awali tulipanga na marafiki zangu kadhaa wa karibu wa fani tofauti ili tuanzishe kampuni yetu kwa kuwa huduma zetu hazihitaji mtaji mkubwa bali ni samani za ndani na kulipia ofisi,lakini tulipo maliza wengi waliogopa na kudai kuwa kozi zao zinauzika mjini kwa hiyo bora wakafanye kazi za kuajiriwa na tukabaki wawili lakini mchakato wetu unaendelea vizuri.
  Naombeni tusiwe na mawazo ya kutafuta mamilioni ili tuanzishe ofisi zetu ambazo kwa hizo tutakuwa tumejiajiri!!!!!!
  Msidhani mi ni mtoto wa fisadi kwa kutoa mawazo hayo.....maana ninachokifanya hata mzazi wangu hajui na sijarudi kijijini kwetu ingawa nasisitizwa nirudi kijijini ila ni kubaki hapahapa mjini kubanana mpaka kieleweke
  inawezekanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa wana jf maana ajira imekuwa kilio kwetu,tujiunge ili nasi tutoe ajira kwa hao wenye mawazo bado ya kuajiriwa,waendelee kusubiri
   
 2. m

  mondy New Member

  #2
  Sep 4, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  well said pal.. all the best in your endevours.. hope you will be successfull
   
 3. M

  Malila JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Niungane na wewe kwa kuongeza neno moja, tafsiri ya mtaji haijaeleweka kwa wengi wetu. Nilipofikia uamuzi wa kutaka kujiajiri mwenyewe,niliangalia nguvu nilizonazo kwanza, nikagundua nina nguvu za kufanya mambo yatokee,kwa hiyo nikafuta wazo la kukopa. Niliamua kuipa akili yangu nafasi ili ifanye kazi yake ktk mazingira niliyokuwepo. Milango ikafunguka.
   
 4. ldd

  ldd JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 792
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  its well bt try to summaries your work!!! ndo maana hamna komenti hapa!!!
   
 5. Ikumbilo

  Ikumbilo JF-Expert Member

  #5
  Sep 4, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 455
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mimi hata nikipata pesa siwezi kuajiri mtu, ya nini niwe na headache? Ni bora nikanunua suzuki nadunda nayo mtaani kila mtu ananijua kuwa nami nina usafiri.
   
 6. s

  sirmudy JF-Expert Member

  #6
  Sep 4, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Akili ni nywele, kila mtu ana zake........, ss ukishanunua gari ili iweje...? kwani gari ni nn kwa maisha ya ss.? hata hiyo gari nayo ina headache...., wangapi wana magari na wanayaacha nyumbani kwa kukosa pesa ya mafuta...? Fikiri kwa upana wa fikra na si kwa ufupi wa fikra...!
   
 7. M

  Mwana Mnyonge JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 348
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  ona huyu masubuli matupu
   
 8. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Maelezo meeeengi!!
   
 9. m

  mbasamwoga Member

  #9
  Sep 6, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe unafaa kwa dunia ya sasa, ila usiogope kukopa benki. Bila mkopo hujawa mfanyabiashara wa ukweli....... Nami kama wewe vile. Wazo moja njia moja na mtazamo mmmmmmumojaaaaa
   
 10. R

  Richardbr Senior Member

  #10
  Sep 12, 2011
  Joined: May 29, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  I agree with you lakini shirikisha huo mchakato wako
   
Loading...