Wambugani
JF-Expert Member
- Dec 8, 2007
- 1,757
- 277
Inasikitisha katika Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Endalah tarehe 9 Julai, 2016 mojawapo ya agenda iliyowagusa wananchi ni ya ubinafsishaji wa makorongo ya mchanga pamoja na mita 60 kutoka kwenye korongo.
Hili jambo baya sana,na haliweze kufumbiwa macho na wananchi wenye uzalendo kwani watu hawapo tayari kuingia migogoro na hao wanaoitwa wawekezaji. Kwani kwa miaka yote wananchi wameishi bila kero na kutumia makorongo hayo yenye chemichemi kujipatia maji kipindi chote (perennial) na kupata malisho ya mifugo yao.
Pia mita 60 kutoka makorongo hayo ni makazi na mashamba ya wananchi.
Ni bora sasa viongozi wa Serikali ya Kijiji waache tabia yao ya tamaa ya pesa na kuharibu amani na utulivu wa wananchi kwa kutuletewa mtu ambaye atakuwa kero kwa maisha yao na mali zao!
Wajifunze vurungu zilitokea kutoka maeneo mbalimbali yenye migogoro na wawekezaji.
Mwenendo huo kwa viongozi kutoa maeneo ya wananchi pasipo ridhaa yao ni wa kukemewa