Hakuna wa kumfunga paka kengele! Sasa ni mwendo wa kuchukua ardhi na kuwapa wawekezaji, huku wazawa wakilipwa fidia kwenye ardhi ya mababu zao na kuhamishiwa maeneo yasiyo na rutuba. Kwa mwendo huu, ipo siku Watanzania watapanga kwenye ardhi yao wenyewe kwa sababu ardhi yote imepewa wawekezaji.
Umuhimu wa kurudisha Tanganyika unaonekana wazi sasa, maana hali hii haileti picha nzuri. Bandari zinazorasimishwa zipo Tanganyika, si Zanzibar. Ardhi inayorasimishwa ni ya Tanganyika, si ya Zanzibar. Wananchi wanaoondolewa kwenye maeneo yenye rutuba na ardhi yao kugawanywa kwa wawekezaji ni wa Tanganyika, si wa Zanzibar.
Je, hili ni sawa? Kwa nini hata marais waliopita, kama Jakaya Kikwete, hawakurasimisha mali za Zanzibar kwa mtindo huu?