Ubinafishaji wa Makorongo ya Mchanga Wilayani Karatu

Wambugani

JF-Expert Member
Dec 8, 2007
1,757
276
Inasikitisha katika Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Endalah tarehe 9 Julai, 2016 mojawapo ya agenda iliyowagusa wananchi ni ya ubinafsishaji wa makorongo ya mchanga pamoja na mita 60 kutoka kwenye korongo.

Hili jambo baya sana,na haliweze kufumbiwa macho na wananchi wenye uzalendo kwani watu hawapo tayari kuingia migogoro na hao wanaoitwa wawekezaji. Kwani kwa miaka yote wananchi wameishi bila kero na kutumia makorongo hayo yenye chemichemi kujipatia maji kipindi chote (perennial) na kupata malisho ya mifugo yao.

Pia mita 60 kutoka makorongo hayo ni makazi na mashamba ya wananchi.

Ni bora sasa viongozi wa Serikali ya Kijiji waache tabia yao ya tamaa ya pesa na kuharibu amani na utulivu wa wananchi kwa kutuletewa mtu ambaye atakuwa kero kwa maisha yao na mali zao!

Wajifunze vurungu zilitokea kutoka maeneo mbalimbali yenye migogoro na wawekezaji.

Mwenendo huo kwa viongozi kutoa maeneo ya wananchi pasipo ridhaa yao ni wa kukemewa
 
Inasikitisha katika Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Endalah tarehe 9 Julai, 2019 mojawapo ya agenda ni ya ubinafsishaji wa makorongo ya mchanga pamoja na mita 60 kutoka kwenye korongo.

Hili jambo baya sana,na haliweze kufumbiwa macho na wananchi wenye uzalendo kwani watu hawapo tayari kuingia migogoro na hao wanaoitwa wawekezaji. Kwani kwa miaka yote wananchi wameishi bila kero na kutumia makorongo hayo yenye chemichemi kujipatia maji kipindi chote (perennial) na kupata malisho ya mifugo yao.

Pia mita 60 kutoka makorongo hayo ni makazi na mashamba ya wananchi.

Ni bora sasa viongozi wa Serikali ya Kijiji waache tabia yao ya tamaa ya pesa na kuharibu amani na utulivu wa wananchi kwa kutuletewa mtu ambaye atakuwa kero kwa maisha yao na mali zao!

Wajifunze vurungu zilitokea kutoka maeneo mbalimbali yenye migogoro na wawekezaji.

Mwenendo huo kwa viongozi kutoa maeneo ya wananchi pasipo ridhaa yao ni wa kukemewa
Tarehe umekosea au mimi sijakuelewa
 
Itisheni mkutano wa kijiji chenu haraka isije ikawa ni jambo lililoridhiwa na watu wenu bila wewe kujua mkuu Wambugani
 
mchanga ni madini ujenzi, sheria inaruhusu mtu/watu kumiliki leseni za uchimbaji wa mchanga mitoni. cha msingi ni kuwepo uelewano na sheria kuzingatiwa katika kuendesha shughuli hii. kumbuka madini ni ya serikali japokua eneo laweza kuwa lako. ni muhimu ukafatilia ujue kama anafanya kihalali au la na pia kama kijiji kilimpa mambo ya kutekeleza je anayafanya? kulalamika hakutazuia shughuli hiyo kuendelea sababu mchanga unahitajika sana even locally.
 
Itisheni mkutano wa kijiji chenu haraka isije ikawa ni jambo lililoridhiwa na watu wenu bila wewe kujua mkuu Wambugani
Wananchi walikataa katakata katika mkutano ule. Hivyo, hakuna ridhaa ni sasa kama ilivyokuwa Kijiji cha Chemchem, jirani na Kijiji hicho.
 
Back
Top Bottom