Ubeberu kwenye mikopo elimu ya juu

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,412
7,194
Licha ya kua raia wa kipato cha kawaida tu kuna watu watoto zao hawapewi mikopo ya elimu ya juu kosa lao eti kusoma shule za binafsi.
Inatia uchungu kuona hao hao baraza la mikopo elimu ya juu kuweza kutoa mikopo kwa wanafunzi wasio watanzania. Inaonyesha baraza hilo jinsi walivyo na upendeleo au uzembe. Unakuta mtu bila kutumia uongo na hila au kutoa rushwa hawezi pata mkopo.
Hivi majuzi kumekua na wanyarwanda wamekamatwa kwa kupewa mkopo wa elimu jambo ambalo hawastahili. Sio hao tu kumekua na wageni wengi toka nchi jirani kama vile burundi rwanda kenya uganda na hata malawi wamekua wanasoma kwa mikopo tanzania na kisha kutokomea kwao bila kulipa hata senti moja ya mikopo hiyo.
Katika awamu hii bila shaka mengi ya nyuma yatajulikana kutokana udhibiti kuimarika katika mikopo ya elimu ya juu.
 
Mkuu kama unaweza kusomesha mtoto chuo msomeshe. .....
Jikaze tu kama nguvu zipo mkuu,
Maana balaa la kulipa Hilo den ni kubwa mnoo. ....
Mtayarishie mwanao maisha mazur mkuu....
15% ya GS ni kubwa mnoo. ..
 
Kupewa mkopo na HELSB siku hiz tangu jiwe aingie ni changamoto sana, miaka ya kikwete ilikua mteremko mtu.

Kero ya mkopo wa HELSB ni kuurudsha. Kama nguvu ipo ni mara 1000 mtu asichukue huo mkopo. Kero kero sana
 
Back
Top Bottom